Habari

Wabunge wanaobandika kucha na kope bandia wapigwa marufuku kuingia bungeni

Spika Ndugai

Spika wa Bunge la Jamhuri ya  Muungano wa Tanzania, Job Ndugai amepiga marufuku wabunge kuingia bungeni wakiwa na kucha na kope bandia.

Spika Ndugai akitoa msisitizo wa  tamko  hilo alilolitoa Jana,  amesema ataendelea kupokea maoni pia kuhusu suala la wabunge kuchibua ngozi, huku akisisitiza kuwa ataendelea kuwazuia Wabunge na  wageni watakaotembelea Bunge hilo  walioweka kucha na kope bandia.

Spika Ndugai akifafanua namna ya  ukaguzi huo utakapofanyika kwenye mahojiano yake na BBC amesema “Kuna walinzi wa mageti ya bunge ambao sio tu wataangalia nyusi na kucha lakini pia tuna kanuni zetu za mavazi ambazo huwa zinaangaliwa wakati wote. Mtu ambae anakuja na mavazi ambayo hayakubaliwi kikanuni huwa hakubaliwi kuingia. Sasa katika hayo masharti ya kikanuni limeongezeka hili la kucha na nyusi bandia.”.

Kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa Jana bungeni na Naibu Waziri wa Afya, Dkt Faustine Ndungulile amedai kuwa watu 700 kwa mwaka hupokelewa katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili wakiwa na matatizo ya ngozi yatokanayo na kijichubua.

Ndugai alitoa maamuzi hayo Jana baada ya Mbunge wa Viti Maalaum Mhe. Fatma Toufiq kuihoji serikali juu ya athari za kiafya za matumizi ya kucha na kope bandia pamoja na kujichubua.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents