Habari

Wabunge wanawake kutoka Ukawa wamejitoa kwenye umoja wa Wabunge Wanawake Tanzania (TWPG)

Wabunge wanawake kutoka vyama pinzani wanaounda Ukawa wamejitoa kwenye kwenye umoja wa Wabunge Wanawake Tanzania (TWPG) kutokana na kauli ya Mbunge wa Ulanga, Goodluck Mlinga (CCM) aliyoitoa Bungeni, Mei 5 mwaka huu.

bunge(3)

Mbunge huyo alisema Bungeni, “ili mtu ateuliwe kuwa Mbunge wa Viti Maalumu ndani ya Chadema lazima awe “bebi” wa mtu.”

Kutokana na barua iliyoandikwa Mei 6 na wabunge hao wanawake kutoka upinzani yenye saini ya wabunge hao 53 ilisema, “Licha ya juhudi mbalimbali zilizofanywa na wabunge wa upinzani kutaka mwongozo wa Spika ili Mlinga afute kauli yake, Naibu Spika (Dk Tulia Ackson) alipuuza miongozo hiyo.”

Barua hiyo iliyotiwa saini na Mbunge wa Kawe (Chadema), Halima Mdee akifuatiwa na wabunge hao, imenakiliwa pia kwa Spika wa Bunge, Job Ndugai.

Hata hivyo juzi wakati akichangia hotuba ya Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mlinga alisema anashangaa kila mahali ni Mlinga, Mlinga na kupigiwa simu za vitisho.

“Naamini vyombo vya ulinzi na usalama vitamlinda na kusema kama Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), liliweza kuwachakaza waasi wa M23, basi hawatashindwa kumlinda,” aliongeza.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents