Siasa

Wabunge waridhishwa na utendaji kazi wa Ofisi ya Rais Menejimenti ya umma na Utawala bora

Waheshimiwa wa bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa nyakati tofauti wameelezea kuridhishwa kwao na utendaji wa Ofisi ya Rais Menejimenti ya umma na Utawala bora na taasisi zake kwa kuweza kutoa huduma bora kwa wananchi.

Taarifa iliyotelewa Alhamisi hii na Ofisi ya Rais Menejimenti ya umma na Utawala bora, imeandika kuwa wabunge wameridhishwa na utendaji kazi wa kitengo hicho kama ifuatavyo;

Wabunge wameonyeshwa kuridhishwa huko wakati wakichangia hoja kuhusiana na masuala ya kiutumishi na utawala mara baada ya Waziri wa nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mh Angellah Kairuki (mb) kuwasilisha bungeni makadirio ya matumizi ya fedha kwa mwaka wa fedha 2017/2018 ya Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora na taasisi zake.

Akizungumzia kuhusiana na zoezi la kuwaondoa watumishi hewa katika orodha ya malipo ya mishahara ya Watumishi (payroll), Mh. Abdallah Bulembo (mb) ameipongeza Ofisi ya ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kwa kuondoa watumishi wasiostahili katika orodha ya malipo ya serikali. “Mmewababini na kuwaondoa watumishi hewa 13,000 si jambo, hivyo mnahitaji kupongezwa ,” Mhe Bulembo alifafanua.

Naye Mh.Sadick S.Murad ameipongeza Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kuhakiki kwa wakati madai ya watumishi wa Mvomero na kupelekea serikali kulipa madai yao.

“Nimeridhishwa nawe Waziri Kairuki, kwa usikivu na utendaji kazi wako ambao umewezesha watumishi katika jimbo langu na kulipa madai yao yote,” alisema Mh Murad.

Kwa upande wake Mh.George Lubeleje ameipongeza Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kwa mpango mzuri wa kunusuru Kaya maskini (TASAF) na mpango wa kurasimisha biashara za wanyonge nchini (MKURABITA) ambapo wananchi wa kawaida ni walengwa wamenufaika licha ya kuwa na changamoto ndogo ndogo.

“Kaya maskini zimenufaika kupitia TASAF lakini pia MKURABITA hivi sasa imebadilisha maisha ya wananchi kwani wanakopesheka na taasisi za kifedha kutokana umiliki wa ardhi kupitia hati za kimila ,” alisema Mh. Lubeleje.

Aidha Mh Peter Msigwa akichangia hoja, ameishauru serikali kuhakikisha kuwa Chuo cha uongozi (Uongozi Institute) kinakuwa na mtaala maalum utakaowajengea uwezo viongozi katika kutekeleza majukumu yao kikamilifu.

Na Emmy Mwaipopo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents