DStv Inogilee!

Wachambuzi wataka mgomo wa wafanyakazi uwanja wa ndege Jomo Kenyatta kutatuliwa haraka, wahofia athari za kiuchumi

Mgomo wa wafanyakazi wa uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyatta mjini Nairobi nchini kenya huenda ukaleta athari za kiuchumi kwa wakati ujao na hivyo wachambuzi wa masuala ya kiuchumi wataka utafutwe ufumbuzi wa kudumu.

”Muwekezaji atakayetaka kuwekeza katika usafiri wa ndege atataka kujua ikiwa wafanyakazi hawatamletea hasara kabla ya kuwekeza katika kampuni ya Kenya Airways”.

Kwa mujibu wa Shirika la habari la BBC, Alisema Tony Watimu, katika mahojiano na BBC. Aliongeza kusema ingawa kwa sasa hasara kubwa za kiuchumi hazijajitokeza kwa kiwango cha kuhofia, serikali inapaswa kuchukua hatua zinazofaa kumaliza mzozo huo.

”Hatuwezi kusema mzozo h madhara kubwa kwa uchumi wa kenya.

Serikali ingechukua jukumu kuzungumza na wafanyakazi wanaofany amgomo ili kutatua mzozo. Kutumia nguvu si njia nzuri ya kusuluhisha mzozo wa kikazi”. Alisisitiza Bwana Watima.

Maelfu ya wasafiri wa ndege waliokuwa wakisafiri maeneo tofauti duniani walijipata bila pa kwenda siku ya Jumatano baada ya wafanyikazi wa uwanja wa ndege wa kimataifa wa JKIA nchini Kenya kugoma.

Polisi waliwasili na kuwatawanya wafanyikazi hao kwa vitoa machozi huku baadhi yao na hata wasafiri wakipata majeraha madogo katika purukushani hilo.

Mgomo wa wafanyakazi watatiza usafiri katika uwanja wa ndege JKIA

Kiongozi wa wafanyikazi hao Moss Ndiema alimatwa na baadaye na kufikishwa mahakamani kwa kuongoza mgomo usio halali kwani mahakama ilikuwa imetoa uamuzi usitishwe.

Masaa sita baadae, wengi wa wasafiri walikua hawajapata suluhu kwasababu safari nyingi zilikuwa zimefutiliwa ama kucheleweshwa.

Wengine walipelekwa katika hoteli mbali mbali wasijue hatma yao.

Hata hivyo ilikuwa afueni kwa baadhi yao baada ya wanajeshi wa anga wa KDF kuletwa ili kusaidia katika ukaguzi.

Mgomo huo umeathiri pakubwa ndege kadhaa na maelfu ya abiria.

Hakuna ndege yoyote iliyotua katika uwanja huo mkubwa katika kanda ya Afrika mashariki ambao unaohushughulikia ndege za abiria 120 kila siku.

Athari za mgomo huu ni zipi?

Afisa mkuu mtendaji wa KQ Sebastian Mikos amesema kuwa safari 24 za ndege zimeathirika kutokana na mgomo huo.

”Tumekuwa tukiwasiliana na wafanyakazi wote wa KAA tangu saa kumi asubuhi, kwa kweli ni kweli shughuli katika uwanja wa JKIA na viwanja vengine nchini zimeathirika kutokana na mgomo huu kwa wakati huu tutasema kwamba safari za ndege zimechelewa… safari za ndege 24 zimeathirika” alisema bwana Mikos.

Baadhi ya abiria

Aliongeza kuwa anaongea kwa niaba ya shirika la ndege ya Kenya.

”Wakuu wengine wa Kampuni za ndege huenda wamechukua maamuzi tofauti kwa kutua katika viwanja vingine au kusitisha safari.”

Waliyoathirika zaidi na mgomo huo ni abiria ambao walikwama kwa saa kadhaa.

”Tumepata shida nyingi ya usafiri hapa, ndege yangu ilikuwa ya usiku wa manane iliahirishwa hadi saa mbili asubuhi mbili na mpaka sasa sijui safari itakuwa ya saa ngapi” alisema mmoja wa wasafiri

Abiria wengine walikabiliwa na matatizo ya kiafya.

Abiria mgonjwa

Abiria waliotarajia kusafiri kutoka kwa uwanja wa ndege wa Moi jijini Mombasa walikwama kwenye uwanja huo wa ndege wakisubiri kupewa maelekezo zaidi na wahudumu wa uwanja huo.

Baadhi yao walilazimika kufutilia mbali tikiti zao kwa muda.

Wafanyikazi hao wamegoma kupinga pendekezo la uongozi wa uwanja huo,ambAo ni wa nne kwa ukubwa barani afrika kupewa kampuni ya ndege ya Kenya Airways.

Wanadai kuwa Kenya Airways inamilikiwa pakubwa na watu binafsi na kuwa wanahofia kupoteza kazi zao iwapo hilo litatendeka.

Madai haya yalikuwa yakichuunguzwa na kamati ya bunge kuhusu uwekezaji ila spika wa bunge la kitaifa Justin Muturi alisitisha uchunguzi huo.

Ni ndege chache tu zilizofanikiwa kusafiri huku safari za ndege zingine zikifutiliwa mbali

Awali katika taarifa yake, Muungano huo wa (Kawu) umesema kwamba ” ni makosa kabisa, na pia uhalifu, kufikiria kwamba KQ itadhibiti JKIA.”

Waziri wa uchukuzi nchini Kenya James Macharia ametaja mgomo huo kuwa haramu na kuuita ‘hitilafu’ kidogo tu na kwamba shughuli za kawaida zitarejea muda mfupi ujao.

Bwana Macharia amesema wizara yake inafanya kila iwezalo kuutatua mgomo huu.

Huku hayo yakijiri shirika la ndege la Morocco, Royal Air Maroc (RAM), limethibitisha kufutlia mbali ndege zake kutoka Casablanca-Nairobi-Ndjamena (Chad).

Shirika hilo limechukua hatua hiyo miaka mitatu baada ya kuzindua huduma zake.

Taarifa kutoka shirika la ndege la Morocco

Wakati huo huo shirika la ndege la Kenya Airways limetoa wito kwa wasafiri kuepuka uwanja huo au kubadilisha ndege zao bila gharama yoyote.

Kenya Airways inamilikiwa kwa 48.9% na serikali na 7.8 % na kampuni ya ndege Air France-KLM.

Ndege 25 za nchi za nje hudumu nje ya uwanja mkuu wa ndege Nairobi, ikiwemo Turkish Airlines, Emirates, South African Airways na Ethiopian.

Kenya Airways ambayo imekuwa ikipata hasara ya mamilioni ya dola katika miaka michache iliyopita ilikuwa ikitarajia kuwa ingefaidi kutokana na kuchukua uongozi wa uwanja huu unaounda faida ya zaidi ya dola milioni mia moja za marekani kila mwaka.

Uwanja wa JKIA hupokea ndege 126 za wasafiri na 25 za mizigo kila siku.

Wasafiri 18,000 wanasemekana kutumia uwanja huo kila siku.

Pia inachangia 83% ya mapato inayopata mamlaka ya usimamizi wa viwanja vya ndege.

Related Articles

Back to top button
Bongo5

FREE
VIEW