Michezo

Wachezaji Everton watakiwa kujifunza lugha ya Kiingereza, Spurs kupambana kumbakisha Harry Kane

Mkufunzi wa Everton, Carlo Ancelotti ameshauri kikosi chake kipya cha kiufundi kujifunza Kiingereza wanapojianda kuzoea Premier League. (Guardian)

Carlo AncelottiMkufunzi wa Everton Carlo Ancelotti

Aston Villa wanamtaka kiungo wa kati wa Marseille Morgan Sanson, 25, lakini nafasi yao ya kumsajili kiungo huyo wa kimataifa wa zamani wa Ufaransa wa chini ya miaka -21 itategemea kama wataponea kuondolewa katika Ligi kuu ya Uingereza. (Birmingham Mail)

Tottenham watalazimika kufanya kila liwezekanalo wasimpoteze mshambuliaji wao Harry Kane, 26, msimu wa joto ikiwa watakosa kufuzu kwa Champions League msimu ujao. (Telegraph)

England's Harry Kane

Mkufunzi wa Spurs, Jose Mourinho amesema hana mpango wa kufanyia marekebisho kikosi chake. (Evening Standard)

Barcelona wameungana na Liverpool na Real Madrid katika kinyang’anyiro cha kumsaka winga wa miaka 20 wa Valencia Ferran Torres. (El Mundo Deportivo via Daily Mail)

Real Madrid wamemuomba meneja wa zamani wa Spurs Mauricio Pochettino kuwafahamisha kuhusu shughuli zake kwa sababu wanataka achukue nafasi ya Zinedine Zidane. (Independent)

Mshambuliaji wa Manchester United, Alexis Sanchez, 31 atalazimika kukubali kupungua kwa mshahara wake ikiwa anataka kuhamia Inter Milan msimu huu wa joto. (Tuttosport via Daily Mail)Alexis SanchezMshambuliaji wa Manchester United Alexis Sanchez

West Ham will firm up their interest in Brentford’s 22-goal striker Ollie Watkins, 24, in the summer if the Bees are not promoted to the Premier League. (Sun)

Mmiliki Cardiff City Vincent Tan ameripotiw kuuza nusu ya hisa zake katika klabu ya Los Angeles FC inayoshiriki ligi ya MLC – na kwamba ana mpango wa kuuza nusu ya hisa zilizobakia. (LA Times)

Tetesi Bora Jumanne

Kiungo wa kati wa Ufaransa Paul Pogba, 26, atarejea katika mazoezi ya kikosi cha kwanza Manchester United wiki hii na anapania kubuni ushirikiano uwanjani na Bruno Fernandes aliyejiunga na klabu hiyo Januari. (ESPN)Paul Pogba kurejea katika mazoezi ya kikosi cha kwanza Manchester United wiki hiiPaul Pogba kurejea katika mazoezi ya kikosi cha kwanza Manchester United wiki hii

Manchester United wanaongoza katika kinyang’anyiro cha kumsajili mshambuliaji wa Borussia Dortmund Muingereza Jadon Sancho, 19, kwa bei inayotarajiwa kuvunja usajili wa katika ligi kuu ya Premia msimu wa joto. (Telegraph)

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents