Michezo

Wachezaji nyota wa Simba watinga katika ofisi za SportPesa (Video)

By  | 

Wachezaji wa klabu ya soka ya Simba na viongozi wao hapo jana siku ya Alhamisi wamewatembelea wadhamini wao wakuu ambao ni kampuni ya kubashiri matokeo ya SportPesa.

Msafara huo uliyobisha hodi katika Ofisi za SportPesa ulikuwa na baadhi ya viongozi wa klabu hiyo pamoja na wachezaji wake wakati lengo kuu ikiwa ni kuona na kutambua namna wadhamini hao wanavyofanya kazi zao huku kikosi cha timu hiyo kikipata semina ya namna wanavyoweza kutumia mitandao yao ya kijamii katika kujiongezea thamani itakayowawezesha kujipatia kipato nje ya fani zao.

Jiunge na Bongo5.com sasa

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Bongo5!

Add a comment

comments