Soka saa 24!

Wachezaji tisa ni majeruhi, Manchester United ikielekea kuwakabili vinara wa ligi Liverpool 

Klabu ya Manchester United inakabiliwa na wachezaji wengi majeruhi kuelekea mechi yao ya Premier League dhidi ya Liverpool siku ya Jumapili, hii ni baada ya meneja wa timu hiyo Jose Mourinho kuthibitisha kuwepo na wengine wawili baada ya kumalizika kwa mchezo wao klabu bingwa barani Ulaya dhidi ya Valencia.

Miongoni mwao, majeruhi saba walibaki jijini Manchester wakati mashetani hao wekundu wakisafiri kwenda kuwakabili Valencia kwenye mchezo wao wa mwisho wa Champions League wakati, Marcos Rojo akilazimika kutoka. Mourinho akimtoa Scott McTominay kufuatia kiungo huyo kupata majeraha wakati wa mazoezi.

Victor Lindelof aliyetokea Benfica mwaka 2017 na Alexis Sanchez hawa wote watakosa mchezo huo wa Liverpool na baadhi ya wachezaji wengine watano wakiwa katika sintofahamu wakiwemo Luke Shaw, Chris Smallin wakati Matteo Darmian na Anthony Martial walikosekana pia kwenye ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya Fulham siku ya Jumamosi iliyopita.

Diogo Dalot aliyetajwa kama mchezaji bora wa mchezo huo na Fulham, anasumbuliwa na majeraha na kushindwa kufanya mazoezi wakati United ikijiandaa kuikabili Valencia hapo jana.

Kwa mujibu wa mtandao wa klabu hiyo hawa ndiyo wachezaji wa Manchester United wanaosumbuliwa na majeruhi kwa ujumla wao na huwenda wakakosekana kwenye mchezo wao ujao dhidi ya majogoo wa Anfield.

Diogo Dalot, Matteo Darmian, Luke Shaw, Marcos Rojo, Victor Lindelof, Chris Smalling, Scott McTominay, Anthony Martial, Alexis Sanchez.

Msimamo wa ligi kuu Uingereza

Related Articles

Back to top button
Bongo5

FREE
VIEW