Wachezaji wa Barcelona, Atletico na Real Madrid waweka rekodi ya kipekee kwenye fainali ya kombe la dunia
Wachezaji wa Barcelona, Atletico na Real Madrid waweka rekodi ya kipekee kwenye mchezo wa fainali ya kombe la dunia
Yakiwa yamebakia masaa kadhaa kuanza kwa mchezo wa fainali ya Kombe la Dunia 2018 nchini Urusi , tayari klabu kubwa tatu kutoka Hispania wachezaji wao watashinda kombe hilo kwa namna yoyote ile.
Klabu ya Barcelona , Real Madrid na Atletico Madrid ndio klabu zilizotoa wachezaji wengi kwenye mchezo wa fainali kati ya Croatia na Ufaransa, wachezaji watatu kwa kila timu.
Wachezaji wa Barcelona watakaotumikia leo timu zao za taifa ni Samuel Umtiti , Ousmane Dembele wote Ufaransa na Ivan Rakitic wa Croatia.
Wachezaji kutoka Real Madrid ni Luka Modric na Mateo Kovačić wote wa Croatia huku Raphael Varane akiitumikia Ufaransa.
Kwa upande wa Atletico Madrid , wachezaji watakaoiwakilisha klabu hiyo kwenye mchezo wa fainali ni Sime Vrsaljko kutoka Croatia na Lucas Hernandez na Antoine Griezmann wote wa Ufaransa.
Katika maana nyingine ni kwamba klabu hizo kwa matokeo yoyote yale ni lazima wachezaji wao wachukue kombe la Dunia leo.