Jiunge ufaidi miezi 2 bure!

Wachezaji wa Brazil walichomfanyia Coutinho kwenye birthday yake (+Picha)

Wachezaji wa timu ya taifa ya Brazil wamesherehekea siku ya kuzaliwa kwa kiungo wao, Philippe Coutinho kwa kumpiga na mayai huku wakimwagia unga baada ya kutimiza miaka 26 hii leo Juni 12.

Kikosi hicho kilichopo nchini Urusi kikijiandaa na michuano ya kombe la Dunia kimetumia muda wake kumuunga mkono nyota huyo wa Barcelona kwenye sherehe hiyo kwa kumpiga na mayai huku wakimwagia unga ikiwa kama sehemu ya tamaduni ya watu wa Brazili.

Zifuatazo ni picha zinazoonyesha matukio ya sherehe hiyo ya kiungo mshambuliaji wa klabu ya Barcelona na timu ya taifa ya Brazili, Philippe Coutinho.

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW