Michezo

Wachezaji wa Japan wapokewa kifalme Tokyo (+Picha)

Maelfu ya washabiki wamejitokeza kwenye uwanja wa ndege wa New Tokyo kuipokea timu yao ya taifa ya Japan ambayo imerejea kutoka kwenye mashindano ya kombe la dunia yanayo endelea huko nchini Urusi.

Japan ilifanikiwa kutinga hatua ya 16 bora ya michuano hiyo na kuweka historia ya kuiyongoza timu ya Ubelgiji kwa jumla ya mabao 2 – 0 kabla ya mashetani hao wekundu kuyasawazisha na kuchomoza na ushindi dakika za lala salama.

Miamba hiyo ya soka barani Asia imejizoelea umaarufu mkubwa pamoja na mashabiki wao kutokana na tabia njema waliyoonyesha kwenye michuano hiyo kwa kufanya usafi kwenye vyumba vyao na hata kusafisha uwanja ambao wameutumia baada ya mechi.

Licha ya kufanya vizuri kwenye michuano hiyo meneja wa kikosi cha Japan,  Akira Nishino utakuwa ndiyo mwisho wake wa kukinoa kikosi hicho.

Shirikisho la soka la Japan (JFA ) limethibitisha hilo hii leo kuwa Nishino hatoendelea na majukumu yake kama kocha wa timu hiyo ya taifa.

Hundreds of Japan supporters welcomed home their team from the 2018 World Cup in Russia

Captain Makoto Hasebe speaks at a press conference held inside the airport on Thursday 

 

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents