Michezo

Wachezaji wa Liverpool wamuunga mkono James Milner (Picha)

Wachezaji wa klabu ya Liverpool wakiwa na wapenzi wao hapo jana siku ya Jumapili wamemuunga mkono mchezaji wa timu hiyo, James Milner katika sherehe ya taasisi yake ya kusaidia vijana yenye lengo la kukuza, kuendeleza na kutoa fursa kupitia michezo ya mpira ikiwemo Mpira wa miguu, Rugby na Kriketi katika kuimarisha afya zao.

James Milner na mpenzi wake Amy Fletcher katika Lost World Charity Ball hapo jana siku ya Jumapili

James Milner mwenye umri wa miaka 31, anamiliki taasisi ya vijana ya michezo yenye lengo la kuimarisha afya zao.

Kati ya wapenzi walihudhuria hapo jana ni pamoja na straika wa Liverpool, Danny Ings akiwa na mpenzi wake Georgia Gibbs

Milner anaecheza nafasi ya winga, kiungo na beki wa kushoto ndani ya klabu ya Liverpool anamiliki taasisi hiyo inayojulikana kama Lost World Charity Ball ambayo hapo jana aliwaalika wachezaji wenzake pamoja na meneja Jurgen Klopp.

Meneja wa Liverpool, Jurgen Klopp na mke wake Ulla Sandrockwakijiunga na ‘party’ jijini Manchester

Adam Lallana na mke wake Emily Jubb wakionekana katika ‘styl’ ya kipekee wakiwasili 

Mlinda lango wa Liverpool, Simon Mignolet akiwasili na mkewake Jasmien Claes

Mignolet si mlindalango pekee aliyewasili hapo bali hata golikipa namba moja nchini Uingrereza , Joe Hart na mkewake Kimberley wakiwasili katika sherehe hiyo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents