Michezo

Wachezaji wa Singida United wafurahia udhamini wa SportPesa

Wachezaji wa Singida United wamekuwa na shauku kubwa yakufanya vizuri ndani ya msimu wako wa kwanza ili kumshawishi mdhamini wao SportPesa kuongeza muda wa kuwadhamini.

Wachezaji wa Singida United wakiwa mazoezini

Kwa sasa kampuni hiyo ya kubashiri, imeingia mkataba wa mwaka mmoja na timu hiyo ambayo tayari imeanza kuonyesha dalili nzuri za kufanya vizuri katika msimu ujao.

Haya ni maoni ya wachezaji hao dhidi ya SportPesa.

Nizar Khalfan –Nahodha

Kikubwa nawaomba SportPesa wasichoke na hatutaweza kuiachia hii nafasi kwani tumepata udhamini wa mwaka mmoja kwahiyo tunaamini watatuongeza mkataba kutokana na upinzani tutakaouleta kwenye ligi kwasababu tutakuja kufanya kitu kikubwa sana.

Tunajua tuna mkataba wa mwaka mmoja na tunataka kuongeza miaka mingine mbele kwahiyo hatutaweza kuiachia hii nafasi

Wadhamini wanatusaidia sana kwa sasa kwasababu tumepata jezi na vifaa vingine vingi vya mazoezi kwahiyo sisi wachezaji tunatakiwa kupiga kazi, hivyo wao kama wadhamini wana mchango mkubwa kwenye timu.

Atupele Green

Udhamini ni mzuri, unaleta hamasa katika timu na umesaidia benchi la ufundi kuweza kufanya usajili mzuri kwenye timu ili kuleta changamoto katika ligi yetu

Elisha Muroiwa (Nahodha Msaidizi) (Raia wa Zimbabwe)

Tunashukuru kwa kile wanachokifanya kwa timu naudhamini wao unavutia wachezaji wengi wazuri kujiunga na timu yetu husuani pale wanapoona timu ina wadhamini wakubwa kama SportPesa

Source: SportPesa News

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents