Wachezaji wanne kati ya 12 waliyokwama mapangoni nchini Thailand waokolewa (+Picha)

Jumla ya wachezaji wanne wa timu ya vija waliyokwama kwenye mapango ya Chiang Rai nchini Thailand wamepata bahati ya kuokolewa hapo jana siku ya Jumapili kati ya wachezaji soka 12 waliyozama.

Kwa mujibu wa chombo cha Al Jazeera taarifa za hivi karibuni zinaeekeza kuwa jumla ya wanachama nane wa klabu hiyo ya soka ya vijana bado wamekwama kwenye mapango hayo ya kaskazini mwa nchi ya Thailand.

Jumla ya vijana wanne kati ya 12 waliyookolewa wamewahishwa kwenye hospitali ya Chiang Rai, iliyopo kilomita 60 kutoka maeneo hayo kwaajili ya matibabu zaidi.

Vijana hao wa kiume wamekwama tangu June 23 mwaka huu wakiwa walikwenda na waalimu wao kwaajili ya kutembelea mapango hayo kablaya kujaa maji.

Dunia nzima imeungana na Thailandi hii leo siku ya Jumatatu kwaajili ya kusaidia zoezi hilo kwenda kama linavyo tarajiwa huku wazazi wa watoto hao wakiendelea na maombi.

Image result for Four Soccer in Thailand

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW