Habari

Wachina wawili watimuliwa nchini

Uongozi wa Mkoa wa Morogoro umewakamata raia wawili kutoka nchini China na kuwaamuru kurejea kwao baada ya kukaidi mara kadha amri zilizokuwa zikiwataka kusimamisha shughuli walizokuwa wakizifanya kinyume cha sheria katika kiwanda wanachokimiliki cha Marumaru cha Zhong Fenq kilichopo katika kijiji cha Maseyu.

Hatua hiyo inakuja baada ya Waziri mkuu, Kassim Majaliwa kutoa agizo kutokana na malalamiko ya Mbunge wa Morogoro Kusini Mashariki, Omary Mgumba kuwa wawekezaji hao kutoka China wanaendesha shughuli za uchimbaji bila ya kuwa na kibali.

Mgumba alieleza kuwa tangu mwaka 2010 wawekezaji hao wameendesha shughuli zao bila kulipa kodi za Serikali, hivyo kuikosesha Serikali mapato.

Majaliwa alisema iwapo wahusika watabainika kuwa hawajafuata sheria, kanuni na utaratibu hatua zichukuliwe dhidi yao ikiwa ni pamoja na kuwaondoa katika eneo hilo chini ya ulinzi na kuwasiliana na ubalozi wa China nchini.

Hatimae, Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Dkt Stephen Kebwe alitoa agizo kwa vyombo vya ulinzi kuwakamata raia hao na kuamuru warudishwe nchini kwao baada ya kufanya kazi bila kufuata utaratibu,sheria na kanuni za nchi.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents