Michezo

Wafahamu Mabingwa wa ligi za Ulaya na Bongo 2017

Tukianzia hapa nchini, katika msimamo wa ligi kuu ya Vodacom, klabu ya soka ya Yanga inaongoza ligi ikiwa na alama 62, ikiwa imecheza michezo 27. Yanga inaongoza ligi kwa kutofautiana na klabu ya Simba Sc magoli ya kufungwa na kufunga, na mpaka sasa yanga imebakiza michezo 3 katika msimamo wa ligi huku Simba ikiwa imesalia na michezo 2 peke kwa maana hiyo klabu ya soka ya Yanga ina nafasi kubwa ya kuwa mabingwa Msimu huu.


Kabla ya mechi ya Yanga na Kagera suga, ambapo yanga alishinda.

Tukihamia nchini Uingereza, klabu ya Chelsea ndio inayoongoza ligi kuu nchini Uingereza ikiwa na alama 84 ikifuatiwa kwa ukaribu na klabu ya Tottenham Hotspurs yenye alama 77, mpaka sasa The blues imeshajitupa uwanjani mara 35, huku wapinzani wao Spurs wakiwa wameingia uwanjani mara 35. Kwa maana hiyo, klabu ya Chelsea inahitaji alama 3 pekee ili waweze kutangaza ubingwa wa ligi hiyo pendwa zaidi Duniani.

Kwa upande wa huko nchini Hispania, vita kali ya kuwania Ubingwa kwa msimu huu ilikuwa ni kwa klabu ya Bernabeu, vijana wa kocha Zinedine Yazzid Zidane maarufu kama “ ZIZOU” kocha kijana na mwenye bahati kubwa, akiiongoza klabu iliyomlea na mpaka kufikia hatua ya kumuamini na kumpatia nafasi ya ukocha wa klabu hiyo yenye mapato makubwa kibisa duniani, Real Madrid na Barcelona bado zinaufukuzia ubingwa wa La liga.

Barcelona, inaongoza kwa tofauti ya magoli dhidi ya wapizani wake Real Madrid, lakini klabu ya Real Madrid inapigiwa upatu mkubwa kuwa inaweza kuchukua ubingwa Msimu huu kwa kuwa ina wazidi wapinzani wao mchezo mmoja mkononi, imecheza michezo 35 na ina alama 84 mpaka sasa sawa Barcelona yenye alama 84 na kushuka dimbani mara 35, klabu ya Real Madrid ikiwa imesalia na michezo 3 mkononi huku Barca wakiwa na michezo miwili peke.

Nakunako Ligi 1, nchini Ufaransa klabu ya Monaco imeweza kuvunja ubabe wa muda mrefu uliokuwa nao klabu ya Paris Saint German katika ligi hiyo, mpaka sasa klabu ya Monaco ndio inayoongoza ligi kwa kuwa na jumla ya alama 86 ikiwa imeshuka dimbani mara 35, huku klabu ya PSG ikiwa na alama 83, na ikiwa imebakiza michezo 36. Klabu ya Monaco ndio inapigiwa upatu wa kunyakuwa ubingwa wa msimu huu.

Na huko Ujerumani katika ligi ya bundas liga klabu ya Bayern Munich inaongoza katika msimamo wa ligi ambapo mpaka sasa imejikusanyia jumla ya alama 77 na kuingia dimbani mara 32 dhidi ya klabu ya Rb Leipzig yenye alama 66, iliyocheza jumla ya michezo 32.

Na huko nchini Italia katika ligi ya Seri A, klabu ya Juventus inaongoza ligi hiyo kwa kuwa na jumla ya alama 85,ikishuka dimbani mara 35, dhidi ya mpinzani wake wa karibu klabu ya Roma yenye alama 78 na kushuka dimbani mara 35 sawa na klabu ya Juventus, mpaka sasa Juventus ndio mabingwa wa Seria A kwa mujibu wa ligi hiyo mpaka sasa.

Na huo ndio misimamo ya ligi mbali mbali Barani ulaya pamoja na Bongo kwa Msimu wa mwaka 2017/18.
Na hii ni Ratiba ya Ligi kuu nchini Uingereza katika wiki hii.

BY HAMZA FUMO

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents