AFCON 2019 Tupogo!
Vodacom Data Datani!

Wafahamu vijana waajabu kwenye mazoezi walioingia kwenye kitabu cha Guinness

Je ni mwanamichezo gani ambaye unamfahamu anatumia masaa mengi kufanya mazoezi? Basi wafahamu vijana wawili ambao wanafanya mazoezi kwa masaa sita kila siku.

Unaweza ukawa umeshangaa kutokana na hilo la kushtuka kidogo lakini huo ndio ukweli. Vijana hao ambao wanatoka nchini Vietinam na kuunda kundi la Giang Brothers Co, 34, na Nghiep, 28 katika mchezo wa ukakamavu hutumia masaa hayo kufanya mazoezi ambayo kwao yamekuwa kama chakula.

Co na Nghiep japo wamekuwa sio maarufu sana duniani lakini wamewahi kushinda tuzo kibao katika mataifa tofauti tofauti ikiwemo nchini kwao Vietinam, Urusi, Itali, China na sehemu nyingine.

Kama hilo halitoshi basi chukua na hili kubwa zaidi – Mwaka jana walifanikiwa kuinga kwenye kitabu cha Guinness World Records kinachoonyesha maajabu lukuki ya watu waliyowahi kufanya na rekodi zao.

Lakini umaarufu wa vijana hao umeanza kuonekana kipindi hiki kwenye mashindano ya Britain’s Got Talent 2018.

Katika onyesho la mashindano hayo walilofanya mwezi April vijana hao waliwaacha midomo wazi mashabiki pamoja na majaji wao Simon Cowell, Amanda Holden, Alesha Dixon na David Walliams.

Majaji hao walishangazwa na uwezo wa vijana hao ndipo Amanda alipowauliza kwanini wamekuwa na nguvu hivyo? “Tunafanya mazoezi kila siku kwa saa 6 kwa siku,” wamejibu vijana hao.

Naye Jaji David aliuliza ni mudagani wamekuwa wakifanya mazoezi hayo? Walijibu kwa kusema tangu walipokuwa na umri wa miaka 10.

Related Articles

Back to top button
Bongo5

FREE
VIEW