Michezo

Wafahamu wachezaji 10 bora wa Tenis kwa upande wa wanaume Duniani

Wafahamu wachezaji 10 bora wa Tenis kwa upande wa wanaume Duniani

Licha ya kushinda taji la Wimbledon jana baada ya kumfunga Kevin Anderson raia wa Africa Kusini kwa seti 6-2 6-2 7-6 na 7-3 Novak Djokovic pia akishinda taji la Australian Open mara 6,French Open mara 1,US Open mara 2,na Wimbledon mara nne bado anashikilia na Nafasi ya 10.

Kati ya wachezaji 10 bora wa mpira wa Tenis Duniani kwa upande wa wanaume kwa viwango vilivyotolewa na Chama cha mpira wa Tenis Duniani (ATP) akipanda kwa nafasi nne kutoka nafasi ya 14 ya mara ya kwanza,na hii ndio orodha ya wachezaji 10 bora wa kiume pamoja na alama zao.

Namba 1.Bado inaendelea kushikiliwa na Rafael Nadal raia wa Uhispania mwenye alama 9310.
Namba 2. ni Roger Federer raia wa Uswisi akiwa na alama 7080.
Namba 3. inashikiliwa na Alexander Zverev raia wa Ujeruman akiwa na alama 5665,huku
Namba 4. ikishiiliwa na Juan Martín del Potro raia wa Argentina akiwa na alama 5395.
Namba 5. inashikiliwa na mwafrika Kevin Anderson akijikusanyia alama 4655.
Namba 6. ni raia wa Bulgaria Grigor Dimitrov mwenye alama 4610.
Namba 7. imeshikiliwa na Mcroatia bwana Marin Čilić akiwa na alama 3905 huku Namba 8. ikibebwa na Mmarekani John Robert Isner akijikusanyia alama 3720.
Namba 9. akiwa ni raia wa Australia Dominic Thiem akiwa na alama 3665 na
Namba 10. akishikilia bwana Novak Djokovic akiiwakilisha nchi ya Serbia akiwa na alama 3355.hao ndio wachezaji 10 bora wa kiume katika mchezo wa Tenis Duniani.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents