Michezo

Wafahamu wachezaji walioko sokoni Ulaya jumamosi hii, Higuain, Suarez, Morata, Dembele na wengineo

Chelsea imemaliza majadiliano ya kumsajili mshambuliaji wa AC Milan, Gonzalo Higuain, 31, kwa mkopo kutoka Juventus, akiwa pamoja na Alvaro Morata, 26. (Sun)

Milan inafikiria kumuuza mchezaji wa Ivory Coast Franck Kessie, 22, ambaye amekuwa akihusishwa kuhamia Tottenham na Chelsea, kwa euro milioni 45. (Calciomercato)

Ligi kuu ya China ‘Beijing Sinobo Guoan’, imefanya mkakati wa kumsajili kiungo wa kati wa Tottenham, Mousa Dembele, 31. (Sky Sports)

Mchezaji wa Barcelona Denis Suarez, 24, anakaribia kujiunga na Arsenal.

Mchezaji huyo wa Uhispania awali alikuwa amehusishwa na Everton pamoja na West Ham. (Sport – in Spanish)

Meneja wa Unai Emery inaitaka Arsenal kuendelea kuwa na Aaron Ramsey mpaka mwisho wa msimu badala ya kiungo wa kati wa Wales ambaye amekuwa akihusishwa na Juventus, kuondoka mwezi huu. (London Evening Standard)

Bosi wa zamani wa Manchester United na Chelsea, Peter Kenyon bado yuko katika ushindani wa kuinunua Newcastle na tayari amewasiliana na mmiliki Mike Ashley na kuhaidiana kuwa watafanya mazungumzo tena mwezi huu. (Mail)

Kenyon anaamini kuwa mmiliki wa Newcastle yako katika hatua ya juu yenye matumanini. (Newcastle Chronicle)

Liverpool haitamruhusu kiungo wa kati wa England Adam Lallana, 30 kuondoka kwa mkopo mwezi huu. (Sky Sports)

Fenerbahce ilitoa kiwango kikubwa cha mkopo kwa mchezaji huyo wa zamani wa Southampton, Lallana mpaka mwisho wa msimu. (Fotomac, via Express)

Manchester City imeshindwa kumsajili mchezaji wa Toulouse Jean-Clair Todibo, ambaye sasa hivi anatarajia kuhamia Barcelona. (Independen

Mlinzi wa West Ham Reece Oxford, 20, amehusishwa kuhamia Borussia Monchengladbach mwezi huu, ingawa anaweza kusubiri msimu wa kiangazi ili ahamie Arsenal. (Mirror)

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 30 amehusishwa na kuhamia Villarreal, jambo ambalo anaweza kulitimiza akiwa amerudi katika nchi yake.

Kiungo wa kati wa Paris St-Germain, Adrien Rabiot atajiunga na Barcelona bila malipo yeyote katika kipindi hiki cha kiangazi.

ottenham imeongeza nafasi ya kumpoteza mlinzi wa kati, Toby Alderweireld, 29, baada ya kuondoa kifungu kilichokuwa kinatoa Euro milioni 25 licha ya kuongeza mkataba wake. (ESPN)

Vicente Iborra anaweza asirudi Leicester baada ya kupewa muda wa kupumzika na kurejea Uhispania kwa ajili ya familia yake.

Bosi wa West Ham, Manuel Pellegrini amekataa mapendekezo yaliyotolewa na mshambuliaji Andy Carroll na Marko Arnautovic,ambapo wote wanaweza kuondoka katika mwezi huu. (Sky Sports)

Mshambuliaji wa Sunderland Josh Maja, 20 amehusishwa na Tottenham, Manchester City na Southampton, kukataa mkataba mpya na Black Cats. (Talksport)

Mchezaji wa Aston Villa Ross McCormack, 32, anakaribia kurudi katika klabu yake ya zamani ya Motherwell kwa mkopo. (Birmingham Mail)

Torino inajiandaa kumpa mchezaji Watford ikiwa ni sehemu ya mpango wa kumzuia mchezaji wa kimataifa wa Argentina Roberto Pereyra, 27,asiondoke kipindi cha kiangazi . (Tuttosport, via Inside Futbol)

Munir El Haddadi, 23 amekataa nafasi ya kuongeza mkataba wake Barcelona na sasa anajiandaa kuondoka bila malipo msimu wa kiangazi. (ESPN)

Chanzo BBC

By Ally Juma

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents