Michezo

Wafahamu wachezaji walioko sokoni Ulaya jumatatu hii, Manchester, Chelsea, Arsenal, zasuguana

Barcelona wamejitolea kwa hali na mali kuhakikisha kwamba hawamuuzi kiungo wa kati wa Uhispania Denis Suarez, 25, kwa Arsenal mwezi huu. (Mirror)

Wolves wamekamilisha mpango wa kumchukua Tammy Abraham kutoka kwa klabu yake ya Chelsea kwa mkopo hadi mwisho wa msimu. Mchezaji huyo wa kimataifa wa England mwenye miaka 21 anatarajiwa sasa kufanya uamuzi leo Jumatatu kuhusu iwpao atakatisha mkopo wake Aston Villa na kwenda Molineux. (Express and Star)

Manchester United wanamfuatilia kwa karibu beki wa AS Roma kutoka Ugiriki Kostas Manolas, 27, ambaye ana kifungu cha £32m cha kumfungua kutoka kwenye mkataba wake. (Sun)

Meneja wa Manchester City Pep Guardiola amesema kwamba haiwezekano kwa winga raia wa England Phil Foden mwenye miaka 18 kuondoka klabu hiyo kwa mkopo. (Independent)

Arsenal hawatarajiwi kuwasili ofa nyingine kumtaka winga wa AS Roma Cengiz Under ambaye thamani yake inakadiriwa kuwa £45m baada ya ofa yao ya awali ya £35m ya kumtaka mchezaji huyo wa Uturuki mwenye miaka 21 kukataliwa. (Star)

Meneja wa Crystal Palace Roy Hodgson amesema hajapokeza taarifa zozote kumhusu mshambuliaji wa Sunderland Josh Maja – licha ya klabu yake kuhusishwa na ununuzi wa mchezaji huyo wa miaka 20 kutoka England mwezi huu. (Mirror)

Aston Villa wanajiandaa kuwasilisha ofa kumtaka mshambuliaji Mfaransa wa miaka 22 anayechezea Brentford Neal Maupay. (Sun)

Abdulkadir Omur, 19, kiungo wa kati Mturuki anayechezea Trabzonspor ambaye amehusishwa na Liverpool amesema anaweza kufurahia sana fursa ya kujiunga na klabu hiyo ya meneja Jurgen Klopp. (Liverpool Echo)

Mkufunzi mkuu wa Newcastle Rafael Benitez bado hajashiriki mazungumzo yoyote na klabu hiyo kuhusu kuongeza mkataba wake licha ya taarifa kwamba klabu hiyo ilipendekeza kumpa mkataba mwingine wa mwaka mmoja hivi majuzi. (Newcastle Chronicle)

Meneja Eddie Howe anasema Bournemouth huenda wakawanunua wachezaji zaidi mwezi huu hata baada ya kuwachukua Dominic Solanke na Nathaniel Clyne. (Sky Sports)

Barnsley huenda wakawasilisha nia ya kumtaka mshambuliaji wa England mwenye miaka 21 anayechezea Sunderland Andrew Nelson, ambaye amekuwa kwa mkopo katika klabu ya Darlington inayocheza Ligi ya Taifa ya Kaskazini. (Sunderland Echo)

Hibernian wamemfanyia majaribio kipa wa Tottenham Tom Glover na kumpeleka mchezaji huyo wa Australia wa miaka 21 kwenye kambi yao ya majira ya baridi jijini. (Edinburgh News)

Chelsea inatarajiwa kuwasilisha dau la £50m kumunua mshambuliaji wa Paris St Germain na Uruguay Edinson Cavani, 31. (Sunday Express)

Arsenal imeanzisha mazungumzo na Barcelona kuhusu kumsajili kiungo wa kati wa Uhispania Denis Suarez na wana matumiani makubwa ya kumsaini mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 katika dirisha la uhamisho la mwezi Januari. (Observer)

Lakini ,mkufunzi wa Gunners Unai Emery pia anataka kumsaini beki na winga . (Mail on Sunday)

Fulham inakaribia kumsaini mshambuliaji wa Liverpool Divock Origi na wamejiandaa kutoa £15m kumnunua mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23 kutoka Ubelgiji. (Sun on Sunday)

Bournemouth itapinga maombi yoyote kutoka Chelsea kumnunua mshambuliaji wa Uingereza Callum Wilson, 26. (Sunday Mirror)

Chelsea itakosa sana huduma za kiungo wa kati mwenye umri wa miaka 31 Cesc Fabregas, ambaye ni mmojawapo wa wachezaji bora kucheza nchini Uingereza kwa miaka mingi, kulingana na beki wa Brazil David Luiz.

Mchezaji huyo wa Uhispania anatarajiwa kujiunga na klabu ya Monaco ya Ufaransa. (Talksport)

Chanzo BBC.

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents