Michezo

Wafahamu wachezaji walioko sokoni Ulaya, Ramsey, Morata, Ozil, Higuain, Fabregas na wengine

Kiungo wa kati wa Arsenal Aaron Ramsey, 28, ametia saini makubaliano ya awali ya mkataba na Juventus na huenda akajiunga na klabu hiyo ya Italia mwezi huu. (Sport Mediaset kupitia Calciomercato)


Ramsey ndiye mchezaji wa sasa aliyekaa muda mrefu zaidi Arsenal, alijiunga nao 2008

Mkurugenzi wa michezo wa klabu ya Sevilla Joaquin Caparros anasema klabu hiyo huenda ikawasilisha ofa kumtaka mshambuliaji wa Chelsea ambaye zamani alichezea Real Madrid na Juventus Alvaro Morata, 26. (Football.London)

Kwa mujibu wa BBC, Morata angependa kurejea Madrid iwapo ataondoka Stamford Bridge lakini anaweza tu kuruhusiwa kuondoka iwapo Chelsea watampata mshambuliaji mwingine wakati wa dirisha la kuhama wachezaji la Januari. (Sun)

Hatima ya Mesut Ozil Arsenal haitaamuliwa hadi mwisho wa msimu baada ya kiungo huyo wa miaka 30 na klabu hiyo kupuuzilia mbali uwezekano wake kuhama mwezi huu. (Evening Standard)

Chelsea watafanya uamuzi kumhusu mshambuliaji Tammy Abraham kufikia 14 Januari. Mchezaji huyo wa miaka 21 yupo Aston Villa kwa mkopo lakini anaweza kuitwa kurejea klabu yake wiki mbili baada ya dirisha la kuhama wachezaji kufunguliwa kutokana na maelezo kwenye mkataba wake. (Telegraph)

Chelsea wameamua kutomfuata mshambuliaji wa Argentina Gonzalo Higuain, 31, mwezi huu. Mchezaji huyo kwa sasa yupo AC Milan kwa mkopo kutoka Juventus. (Goal)

Cesc Fabregas hatakubaliwa kukamilisha uhamisho wake kwenda Monaco hadi Chelsea wapate kiungo wa kati wa kujaza nafasi ya Mhispania huyo wa miaka 31. (Calciomercato)

Mlinda lango wa Real Madrid Keylor Navas, 32, ambaye amekuwa akihusishwa na kuhamia Arsenal wiki za hivi karibuni, ameongeza muda wa mkataba wake katika klabu hiyo kwa mwaka mwingine mmoja, hadi Juni 2021. (Marca)

Bayern Munich wamewasilisha ofa ya tatu ya zaidi ya £30m wakimtaka kiungo mshambuliaji wa Chelsea Callum Hudson-Odoi, 18. (Sky Sports)

Beki wa Chelsea mzaliwa wa England Gary Cahill, 33, anakaribia kuhamia Fulham kwa mkopo. Klabu hiyo ya London magharibi imemrejesha Timothy Fosu-Mensah kwa Manchester United ili kutoa nafasi ya mchezaji mwingine ndipo waweze kumchukua Cahill. (Love Sport Radio)

Crystal Palace wamewasilisha ofa ya £6.5m kumtaka mchezaji wa Everton na Senegal Oumar Niasse, 28, baada yao kushindwa kumpata mshambuliaji wa Liverpool Dominic Solanke kwa mkopo. (Sun)

Paris St-Germain wamewasilisha ofa ambayo haiwezi kufikiwa na Barcelona kumtaka kiungo wa kati Frenkie de Jong, 21, na beki wa kati Matthijs de Ligt, 19, kutoka Ajax. (Marca)

Leicester wamepokea ofa kutoka kwa Villarreal ya Uhispania wanaomtaka Vicente Iborra, lakini klabu hizo bado hazijakamilisha mazungumzo kuhusu uhamisho wa Mhispania huyo mwenye miaka 30. (Leicester Mercury)

Chelsea wanapanga kutoa £36m kumtaka winga wa PSV Hirving Lozano, 23, anayetokea Mexico. (Calciomercato, kupitia Talksport)

Cardiff na Bournemouth wote wanamtaka beki wa Liverpool Nathaniel Clyne. Bournemouth wanamtaka mkabaji huyo wa miaka 27 kwa mkopo kwa kipindi kilichosalia cha msimu. (Mail)

Kiungo wa kati wa Liverpool Adam Lallana, 30, anatafutwa na klabu ya Fenerbahce ya Uturuki mwezi huu. (Caught Offside)

Meneja wa Tottenham Mauricio Pochettino amekataa kufutilia mbali uwezekano wa kiungo wa kati wa Ubeligji Mousa Dembele, 31, kuihama klabu hiyo mwezi huu. (Football.London)

Pamoja na Dembele, Tottenham wanataka kuwauza pia Fernando Llorente, 33, Vincent Janssen, 24, Georges-Kevin Nkoudou, 23, na Victor Wanyama, 27. (Mirror

Nottingham Forest wamehusishwa na kumnunua winga wa Portsmouth Jamal Lowe, 24. (Nottingham Post)

Meneja wa zamani wa Birmingham na Derby Gary Rowett huenda akalazimika kuzuia kushindwa mechi ya Kombe la FA ugenini Shrewsbury Jumamosi ili kunusuru kazi yake kama meneja wa Stoke. (Telegraph)

Christian Eriksen anagoma kutia saini mkataba mpya Tottenham, huku mkataba wa sasa wa kiungo huyo wa kati wa Denmark mwenye miaka 26 ukitarajiwa kufikia kikomo baada ya miezi 18. (Evening Standard)

Juventus wamethibitisha kwamba wameonyesha nia ya kumtaka kiungo wa kati wa Arsenal Aaron Ramsey, 28, bila kulipa ada yoyote baada ya mkataba wake kumalizika mwisho wa msimu. (Sky Sports)

Wolves wamewasilisha ofa ya £18m kumtaka mshambuliaji wa Chelsea Tammy Abraham, 21, ambaye kwa sasa yupo kwa mkopo katika klabu ya Aston Villa inayocheza ligi ya Championship. (Sun)

Bournemouth watamruhusu mshambuliaji wa England Jermain Defoe kuondoka klabu hiyo Januari. Mchezaji huyo wa miaka 36 amechezeshwa mara nne pekee kama nguvu mpya ligini msimu huu. (Sky Sports)

Chelsea wanapanga kuendelea kuimarisha kikosi chao mwezi huu hata baada ya kumnunua Christian Pulisic. The Blues bado wanamtaka mshambuliaji wa Bournemouth Callum Wilson, 26, na pia wanamtafuta beki mpya. (Mirror)

Liverpool wanapanga kumpa mshambuliaji wa wao Daniel Sturridge, 29, mkataba mpya. (Mail)

By Ally Juma

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents