Burudani ya Michezo Live

Wafahamu wachezaji wanaotikisa usajili katika klabu kubwa England 

Chelsea na Manchester City wanaweza kugeuka kwenye mpango wa kumnasa beki wa kushoto wa Everton, Mfaransa Lucas Digne, 26, ikiwa itakuwa vigumu kumpata Ben Chilwell, 23, anayekipiga Leicester. (ESPN)

Chelsea na Manchester City wanaweza kugeuka kwenye mpango wa kumnasa Mfaransa Lucas Digne

Everton, Liverpool, Manchester City na Manchester United wanatarajia kumshuhudia uwanjani, Leon Bailey, 22, siku ya Jumamosi, wakati ambapo winga huyo wa Bayer Liverkusen akiwa na matarajio ya kuhamia England. (Sky Sports)Msenegali Kalidou Koulibaly ni miongoni mwa wachezaji wanaosakwa na Pep gardiola kuimarisha safu yake ya ulinzi

Msenegali Kalidou Koulibaly ni miongoni mwa wachezaji wanaosakwa na Pep Gardiola kuimarisha safu yake ya ulinzi

Kocha wa Manchester City Pep Guardiola amewaorodhesha wachezaji wa nafasi ya ulinzi ya Napoli, Msenegali Kalidou Koulibaly, 29, mchezaji wa Villarreal, Mhispania Pau Torres, 23, na mchezaji wa Benfica Mholanzi Ruben Dias ,23, akitarajia kufanyia mabadiliko safu yake ya ulinzi. (Times)

Sevilla wanajiandaa kufanya uhamisho wa mkopo wa mlinda mlango wa Chelsea Kepa Arrizabalaga, 25, ambaye mustakabali wake haujajulikana Stamford Bridge.

(Sun)

Eric Bailly news hits Ole Gunnar Solskjaer's transfer plans

Valencia inamfuatilia kwa karibu mchezaji Eric Bailly wa nafasi ya ulinzi

Manchaster United wako tayari kumruhusu Eric Bailly, 26 , kuondoka kwa mkopo msimu ujao wakati Valencia ikimfuatilia kwa karibu mchezaji huyo wa nafasi ya ulinzi. (Sun)

Mlinda mlango anayechezea Manchester United kwa mkopo Dean Henderson, 21, ameitahadharisha klabu kuwa hatasubiri milele kuwa chaguo lao la kwanza, kauli hii imekuja wakati Chelsea ikionesha nia na mchezaji huyo. (Express)Dean Henderson, ameitahadharisha Manchester United kuwa hatasubiri milele kuwa chaguo lao la kwanza

Dean Henderson, ameitahadharisha Manchester United kuwa hatasubiri milele kuwa chaguo lao la kwanza

Chelsea inamfuatilia mlinda mlango wa Lille Mike Maignan, 24 na Alphonse Areola, 27 anayecheza kwa mkopo Real Madrid akitokea Paris St- Germain. (Express

Hatahivyo, Tottenham pia wanafikiria kumnyakua Magnan, huku kocha Jose Mourinho akimtolea macho mchezaji huyo kuwa mrithi wa mlinda mlango wa sasa Hugo Lloris, 33. (Sun)Tim Sherwood anaamini nahodha Jack Grealish, 24, atajiunga na Manchester United msimu huu.

Tim Sherwood anaamini nahodha Jack Grealish, 24, atajiunga na Manchester United msimu huu.

Kocha wa zamani wa Aston Villa Tim Sherwood anaamini nahodha Jack Grealish, 24, atajiunga na Manchester United msimu huu. (Birminghma Mail)

imeweka mezani kitita cha pauni milioni 3.5 kwa ajili ya kiungo wa kati wa Reading John Swift, lakini Leeds pia wanamuhitaji mchezaji huyo. (Mail)Jose Mourinho aapa kutomuachilia Giovani Lo Celso

Jose Mourinho aapa kutomuachilia Giovani Lo Celso

Kocha mkuu wa Tottenham Jose Mourinho amesema hatambadilisha Giovani Lo Celso, 24 kwa Bruno Fernandes wa Manchester United, baada ya Spurs kumkosa kiungo huyo msimu uliopita. (Sky Sports)

Sheffield United wangependa kumsajili mchezaji wa nafasi ya ulinzi Abdul Mumin, 22 kutoka FC Nordsjaelland msimu huu. (Mail)

Filip Kostic ,27, anaweza kuondoka Eintracht Frankfurt, huku InterMilan na klabu za rimia zikiwa zinamtolea macho winga huyo raia wa Serbia. (Goal )

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW