Burudani

Wafahamu wanawake kumi walio’date’ na Wizkid

Mara nyingi kumekuwa na list ya kitu ila leo nakutolea list ya wanawake aliowahi kushiriki katika mahusiano ya kimapenzi na staa wa  muziki na mwandishi wa mashahiri kutoka nchini Nigeria, Ayodeji Ibrahim Balogun maarufu kama Wizkid ambaye anafanya vizuri kwa sasa.

Kwa mujibu wa mtandao wa Naijaloaded imetoa orodha ya majina ya wanawake 1o ambao wanadaiwa kujihushisha kwa namna moja ama jingine katika mahusiano ya kimapenzi mastaa kama Huddah, Victoria Kimani, Chiddima wakihusishwa  katika list hiyo.

10. Sophie Ramma
Inasemekena kuwa Sophie Rammal ndiyo alikuwa mpenzi wa kwanza wa msanii huyo baada ya kuingia katika ulimwengu wa muziki na wamewahi kufanya ngoma moja ikifahamika kama ‘Holla at Your boy.’

9. Sola Ogudugu

Sola Ogudugu pia ni moja ya wanawake alikuwa nao msanii huyo katika mahusiano ya kimapenzi na  ikadaiwa kuwa alimpatia ujauzito na ana mtoto mmoja wa kiume wa msanii huo.

8. Tonto Dikeh

Miaka mitano iliyopita kulikuwa na tetesi kuwa Wizkid anatoka na mstaa wa Nollywood, Tonto Dikeh licha ya kuwa wawili hao hawakuwahi kuonekana pamoja na wala kuweka mahusiano yao katika mitandao ya kijamii.

7. Victoria Kimani

Wadakuzi wa mambo walipenyeza habari kuwa msanii kutoka nchini Kenya, Victoria Kimani na Wizkid wapo katika mahusiano ya kimapenzi hii ni baada ya kunashwa picha yao wakidendeka katika Hoteli ya Westlands Kenya.

6. Hudda Monreo

Hamna hasiye juu kuhusu hili, mrembe kutoka Kenya, Huddah Monroe alikutana na msanii huyo mjini Nairobi, ndipo mambo yakamalizwa kuanzia hapo. Huddah hakuficha hisia zake na kuamua kuujuza umma katika mitandao ya kijamii kama ilivyo kawaida yake.when the singer was on tour at the East African country.

5.Chidinma Ekile

Bado list inaendelea na inaelezwa kuwa msanii wa kike kutoka Nigeria , Chidinma ameingia katika orodha hiyo ya kutoka na Star Boy.

Moja ya mahojiano aliyowahi kufanya Wizkid aliwahi kukiri kuwa anampenda Chidinma, “I have a huge crush on Chidinma for a long time…she doesn’t know but it’s true,” alisema Wizkid.

4.Binta Diamond Diallo

Mrembo Binta Diamond Diallo ambaye ni mwanamitindo anaingia katika orodha hii na pia amesha mzalia mtoto msanii huyo, kwani aliwahi kupost vipimo ya DNA mnamo 2016 kuonysha kuwa Wizkid ni baba wa mtoto wake.

3. Seyi Shay

Jina alilopewa na wazazi wake ni Deborah Oluwaseyi Joshua , alizaliwa Desemba 21 mwaka 1985 ila awapo kazini anafahamika kama Seyi Shay. Ni msanii wa muziki na mtayarishaji wa muziki.

Baada ya sura yake kuonekana katika moja ya video za Wizkid  kwa takribani dakika 2:15 ndipo utata ukaanza kutokana na mapozi yake kuwa ya mitego mitego.

2.Tania Omotayo

Huwenda Tania Omotayo atakuwa mwanamke pekee anayependwa na msanii huyo, hii ni baada ya Wizkid kuwa anajing’atang’ata kutoa kauli kuwa yeye na mrembo huyo wameachana ama la, wawili hao wamekuwa katika mahuiano na mara kadhaa penzi lao limekuwa likiingia dhuruba.

1.Justin Skye

Kwa sasa stori zilizopo ni kuwa kijana huyo kutoka nigeria amezama katika penzi jpya la mwanadada Justine Skye, Haman aliyekiri ila kwa mujibu wa mtandao wa mrembo huyo aliposti katikamtandao wa Instagram kuashiria kuna namna.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents