Uncategorized

Wafalme wa nyika, Simba wawili wanyakua tuzo Ulaya

Picha ya Simba wawili, iliyopewa jina la Bond of Brothers (urafiki wa ndugu), imeshinda chagua la Watu katika tuzo za Mpiga Picha Bora wa Wanyama wa Mwaka.

Kwa mujibu wa shirika la habari la BBC, Picha hiyo ilipigwa na David Lloyd, na kuzishinda picha nyengine 45,000 zilizowasilishwa kwenye mchuano huo.

Penguins

Penguin Wafalme’ watatu katika fukwe ya visiwa vya Falkland iliyopigwa na Wim Van Den Heever.

Picha 25 ziliorodheshwa na Makumbusho ya Historia ya Historia ya Asili ili watu wachague wanayoipenda zaidi.

Urban fox

Mbweha akitembea pembeni ya mchoro wa mbwa jijini London, picha iliyopigwa na Matthew Maran

“Nimefurahi sana picha hii kufanya vizuri. Kwa sababu inaonesha hisia za wanyama na kwamba hilo haliishii kwa wanaadamu tu,” amesema Lloyd, ambaye ni raia wa New Zealand aliyelowea London.

Polar bear

Dubu anayetaabika kwa njaa kaskazini ya Canada, picha iliyopigwa na Justin Hofman

Picha nyengine zilizopata kura nyingi za watu ni:

Painted wolves

Mbwa mwitu watatu wanaogombea mguu wa swala, picha iliyopigwa na Bence Máté

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents