Picha

Wafanyabiashara wa simu walia na serikali

Ikiwa yamebaki masaa kadhaa serikali kupitia TCRA watekeleze ahadi yao ya kuzima simu zote feki, wafanyabiashara wa simu wamekuwa wamezidi kulalamika kutokana na kupungua kwa idadi ya wanunuzi wa simu tangu lilipotoka agizo hilo.

phon

Tanzania ni miongoni mwa nchi za kusini mwa Jangwa la Sahara zinazoongoza kwa idadi kubwa ya kuwa na simu feki jambo ambalo liliisukuma serikali kuchukuwa hatua ya kutoa agizo kuwa ifikapo Juni 16 simu hizo zitakuwa hazifanyi kazi tena [zitazimwa].

Aidha kutokana na utafiti nilioufanya nimegundua kuwa tangu serikali ilipotangaza agizo hilo la kuzima simu feki idadi ya wanunuzi wa simu kwenye maduka mbalimbali yamepungua kutokana na wengi wao kuogopa kuwa wanaweza kununua simu na baada ya muda mfupi wakapata hasara ya kuzimwa.

Wakiongea kwa nyakati tofauti na Bongo5, mmoja wa wafanyabiashara wa simu amesema kuwa agizo la serikali ni zuri kwa manufaa ya nchi lakini pia limesababisha hasara kubwa kwao kutokana na kupungua kwa asilimia kubwa ya idadi ya wateja japo simu wanazouza ni original lakini wengi wamekuwa wakiogopa kununua simu hizo kutokana na kuhofia kuzimika.

Aidha naye mkazi mmoja wa jiji la Dar es Salaam, amesema kuwa hilo linatokana na wananchi wengi kutokuwa na elimu ya kutosha ya kujua simu feki na original ndiyo kimechangia kuwa waoga wa kununua simu kwa sasa mpaka pale watakapoona TCRA wamezima simu zote feki na wao ndiyo watapata jibu la kujua simu ipi feki na ipi inafaa kwa matumizi [original].

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents