Habari

Wafanyakazi 14 wa Quality Group wafikishwa kortini

Wafanyakazi 14 wa kampuni ya Quality Group iliyo chini ya Yusuf Manji Jumatano hii walifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kujibu mashtaka matatu likiwemo la kufanya kazi nchini bila ya kuwa na kibali huku waliofikishwa mahakamani ni Meneja msaidizi, mhasibu na washauri 12.

Washtakiwa hao wamesomewa mashtaka mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi, Cyprian Mkeha. Hati ya mashtaka, iliyosomwa na mwendesha Mashtaka, wa uhamiaji Method Kagoma imewataja washtakiwa hao kuwa ni Rojat Surkar, Jagadish Mamidu, Niladri Maiti, Sivarar Raja Sekaran, Mohammed Taher Shaikh, Bijenda Kumar, Prasoon Kumar Mallik na Nipun Dinbandhu Bhatt,Pintu Kumar, Anuj Agurwa, Varun Boloor, Arun Kumar Kateel, Avinash Chandratiwari na Vikram Sankhala.

Akisoma hati ya mashtaka, Kagoma amedai kuwa, Februari 13, mwaka huu, huko katika ofisi ya Quality Group Ltd iliyopo katika Wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam, washtakiwa hao walikutwa wakiwa na viza zilozoghushiwa za kufanyia kazi.

Katika shtaka la pili ilidaiwa kuwa siku na mahali hapo washtakiwa hao wakiwa raia wa India walikutwa wakiishi nchini Tanzania bila ya kuwa na kibali.

Kagoma aliongeza kuwa, Februari 13 mwaka huu, katika jengo la Quality Group washtakiwa hao wakiwa raia wa India walikutwa wakijihusisha na kufanya kazi katika kampuni hiyo kama washauri bila ya kuwa na kibali cha kufanya kazi nchini.

Hata hivyo, washtakiwa hao ambao wanatetewa na mawakili watatu, Alex Mgongolwa na Hudson Ndusyepo wamekanusha kujihusisha na tuhuma hizo na wako nje kwa dhamana baada ya kutimiza masharti ya dhamana na maelezo ya awali watasomewa Machi 7.

By: Emmy Mwaipopo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents