Burudani

Wafanyakazi 6 wa hospitali ya Cedars-Senai wapoteza kazi baada ya kugundulika kuvujisha taarifa za kujifungua kwa Kim Kardashian

Kuvuja kwa taarifa zlilizoupa ulimwengu nafasi ya kufahamu kujifungua kwa staa Kim Kardashian mwezi uliopita kumewatokea puani wafanyakazi sita wa hosptitali ya Cedars-Sinai Medical Center iliyoko Los Angeles, Marekani ambao wamepoteza kazi kwa uzembe wa kuvujisha taarifa binafsi za wagonjwa wa hospitali hiyo.

cedars

Taarifa iliyotolewa na Los Angeles Times (July 13) inadai kuwa mama North West Kim Kardashian ni miongoni mwa wagonjwa 14 ambao taarifa zao binafsi za matibabu za hospitalini hapo zilivujishwa na wafanyakazi hao kati ya kipindi cha( June 18) na ( June 24).

Mke mtarajiwa wa rapper kanye West Kim K alijifungua mtoto wao wa kike June 15 lakini alikuja kutoka hospitali wiki moja baadaye. Baada ya taarifa za kujifungua kwa Kim kuenea mtandaoni vyanzo viliuambia mtandao wa TMZ kuwa familia ya Kardashians ilikuwa inahisi kuna uzembe uliofanyika hospitalini hapo kupelekea kuvuja kwa taarifa hizo sababu Kim hakuwa amemwambia mtu yeyote wa nje taarifa kuhusiana na kujifungua kwake.

Kwa mujibu wa TMZ, Kim Kardashian amefurahishwa na kitendo cha uongozi wa hospitali hiyo kumpigia simu na kumpa taarifa kuwa yeye ni miongozi mwa wagonjwa 14 ambao taarifa zao zilivijishwa, na amefurahishwa na hatua zilizochukuliwa na hospitali hiyo dhidi ya wafanyakazi hao.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents