Habari

Wafanyakazi wa serikali nchini Singapore kuzuiwa kutumia internet kazini

Wafanyakazi wa umma nchini Singapore, hawataweza kupata internet kwenye kompyuta zao wawapo kazini kuanzia May mwakani.

Fund manager
Fund manager

Hatua hiyo imechukuliwa ili kuondoa uwezekano wa email za kazini na nyaraka zinazoweza kutumwa ili kujilinda kiusalama. Maofisa na waajiriwa wa serikali pia watazuiwa kuforward taarifa zozote za kazini kwenye email zao binafsi.

Uamuzi umepingwa vikali mtandaoni. Wengine wanaamini kuwa hatua hiyo itawaathiri pia waalimu ambao kwa kawaida hawazungukwi na taarifa nyeti.

Kama nchi zingine duniani, Singapore imewahi kupata na mashambulio ya kimtandao ikiwa pamoja na shambulio kwenye tovuti ya waziri mkuu mwaka 2013.

Hata hivyo wafanyakazi wataendelea kuwa na email na wataweza kupata internet kwenye vifaa vyao binafsi kama simu nk.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents