Jiunge ufaidi miezi 2 bure!

Wafanyakazi walishwa mende baada ya kushindwa kufikia malengo ya mauzo ya kampuni

Wasimamizi wa kampuni moja ya Kichina wamefungwa jela kwa kuwaadhibu wafanyakazi walioshindwa kufikia malengo ya mauzo kibiashara kunywa mkojo na pia kula mende.

Polisi wamechukua hatua baada ya video kuowaonesha wafanyakazi hao wakichapwa kwa mkanda na kunywa kitu kioevu chenye rangi ya njano ambacho kinadaiwa kuwa ni mkojo.

Mameneja watatu wamehukumiwa kifungo jela kati ya miaka mitano na kumi kutokana na tukio hilo, linaarifu gazeti la Morning Post limearifu.

Video hiyo imekuwa maarufu mitandaoni na watu kutumiana kwa wingi kwenye mitandao nchini China na tovuti mbali mbali ikiwemo tovuti ya Weibo iliyoweka video inayomuonesha muajiri wa kiume akiwa amesimama katikati ya mduara akipigwa mjeledi.

Taarifa za hivi karibuni zinaarifu kuwa kumekuwa na mifano ya kesi kama hizo kwa wafanyakazi kupigana makofi wenyewe kwa wenyewe kwa lengo la kuongeza ari kazini, na wafanyakazi kulazimishwa kutambaa barabarani ama kubusu mapipa ya takataka kama adhabu au kuongeza mshikamano kazi.

Kampuni hiyo pia inaarifiwa kushindwa kuwalipa wafanyakazi wake mishahara kwa muda wa miezi miwili iliyopita, na wafanyakazi walikuwa na hofu ya kuzungumzia suala hilo kwa kuhofia kupoteza malipo yao enapo pia wataacha kazi.

Related Articles

Back to top button
Bongo5

FREE
VIEW