Habari

Wafuasi 13 wa CUF waachiwa huru Kisutu, polisi yawarudia tena

Jeshi la polisi wakishirikiana na askari wa Magereza wametumia nguvu kuwakamata wanachama wa CUF ambao walikuwa wameachiwa huru Jumanne hii katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam.

Wafuasi hao 13 walikuwa wameshtakiwa kwa makosa ya jinai waliachiwa huru na Hakimu Godfrey Mwambapa chini ya kifungu cha sheria namba 225 cha makosa hayo.

Kwa mujibu wa sheria upande wa mashtaka una haki ya kuwakamata tena washtakiwa pale wanapoona inafaa.

Hata hivyo haijajulikana ni idadi ya watuhumiwa hao ambao walifanikiwa kuwatoroka polisi hao.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents