Habari

Wafuasi wa Kenyatta walioandamana mahakamani wavamiwa na kundi la nyuki (+video)

Wakati jopo la majaji watano wa mahakama kuu nchini Kenya wakisoma sababu za kufuta matokeo ya urais nchini Kenya leo mchana jijini Nairobi. Waandamanaji wengi wao wakiwa wafuasi wanaomuunga mkono Rais Uhuru Kenyatta wamelazimika kukimbia kwenye viunga vya mahakama hiyo baada ya kundi la nyuki kuwavamia.

Waandamanaji, Maaskari polisi na Waandishi wa Habari wakiungana kuwatuliza nyuki hao.

Nyuki hao waliotokea kusikojulikana, walionekana kuwaandama waandamanaji hao huku wengi wao wakishindwa kuvumilia na kuanza kutimua mbio.

Mashuhuda wa tukio hilo wamesema watu wengi walikimbia baada ya nyuki hao kuvamia eneo hilo huku mtu mmoja mwenye ulemavu wa miguu akishambuliwa vibaya kabla ya kuokolewa.

Tulimsaidia mwenzetu mwenye ulemavu baada ya kuona nyuki wakimshambulia kwa kasi, hatukujali kama yeye ni mfuasi wa NASA kwani sote ni wakenya,“amesema shuhuda wa tukio hilo aliyejitambulisha kwa jina la Kevin Ochieng kwenye mahojiano yake na NTV.

SOMA ZAIDI – Wanaomuunga mkono Rais Kenyatta waandamana nchini Kenya

Balaa hilo halikuwapata waandamanaji tu bali hata Waandishi wa Habari na Maaskari polisi waliokuwa wakilinda usalama nje ya mahakama nao walishambuliwa na nyuki hao.

Polisi jijini Nairobi wamethibitisha kutokea kwa tukio hilo na ni mtu mmoja tu mpaka sasa aliyeripotiwa kujeruhiwa vibaya na hali yake inaendelea vizuri. Tazama video ya tukio hilo (Video by NTV)

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents