HabariUncategorized

Wafuasi wa upinzani waruhusiwa na mahakama kuandamana nchini Kenya

Mahakama kuu nchini Kenya imeondoa marufuku ya maandamano kwa muda dhidi ya tume huru ya uchaguzi nchini humo (IEBC).

Taarifa hizo zinakuja baada ya Serikali wiki iliyopita kuzuia maandamano yanayotekelezwa na wafuasi wa Muungano wa Vyama vya Upinzani (NASA) kushinikiza mabadiliko ndani ya tume huru ya uchaguzi nchini humo (IEBC).

Hata hivyo, Muungano wa vyama vya upinzani nchini Kenya (NASA) leo umetangaza kuahirisha maandamano, ili kuwaruhusu viongozi wake kuwatembelea watu walioumizwa na polisi wakati wa maandamano.

Kwenye taarifa iliyotolewa na msemaji wa NASA, imeeleza kuwa Raila Odinga na Dennis Onyango watasitisha maandamano leo na kuwatembelea majeruhi. Huku taarifa hiyo ikilaani vitendo vya polisi kuwatawanya wananchi kwa kutumia nguvu.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents