Habari

Wafugaji watakaopitisha mifugo barabara kuu kutozwa faini tsh 300,000/=

Kama wewe ni mfugaji na upo katika Wilaya ya Misungwi mkoani Mwanza kwa sasa utapigwa faini ya shilingi laki 3 kwa kupitisha mifugo barabara kuu.

Image result for ng'ombe barabarani

Uamuzi huo umechukuliwa jana baada ya majadiliano kwenye kamati ya maendeleo ya kata za Lubili, Sumbugu na Isenegeja ambapo Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri Misungwi, Eliurd Mwaiteleke alisema faini hiyo itasaidia kupunguza uharibifu wa barabara unaofanywa na wafugaji.

Barabara nyingi zimeharibika kwa sababu wafugaji wamekuwa wanapitisha mifugo yao, hivyo niwaagize viongozi wote wa vijiji na vitongoji kupitisha ushuru huo ili kukomesha vitendo hivyo,” amesema Mwaiteleke.

Hata hivyo, wananchi wa kata hizo wamekubaliana na agizo hilo na kuwaomba maofisa mifugo kuwaelekeza njia mbadala zitakazotumika.

Aidha, Ofisa mifugo na uvuvi wa halmashauri hiyo, Chrispin Shami amesema kuwa watahakikisha wanapitisha agizo hilo kuwa sheria rasmi ili kuwachukulia hatua kali.

Chanzo:Mwananchi

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents