Habari

Waganda waliotuhumiwa kuua askari, mbwa waachiwa

MAHAKAMA Kuu ya Tanzania Kanda ya Dar es Salaam imewaachia huru washitakiwa wanne kati ya watano Raia wa Uganda waliokuwa wakituhumiwa kuua askari watatu pamoja na mbwa.

Na Grace Michael

 

 

 

MAHAKAMA Kuu ya Tanzania Kanda ya Dar es Salaam imewaachia huru washitakiwa wanne kati ya watano Raia wa Uganda waliokuwa wakituhumiwa kuua askari watatu pamoja na mbwa.

 

 

 

Mahakama iliwaachia huru raia hao wa Uganda mwishoni mwa wiki mbele ya Jaji Thomas Mihayo baada ya Mkurugenzi wa Mashitaka Nchini (DPP) kuwasilisha nolle akiiomba mahakama kuwaachia huru kutokana na kuwa hana nia ya kuendelea kuwashitaki.

 

 

 

Kwa mujibu wa nolle iliyowasilishwa mahakamani hapo, iliwataja washitakiwa ambao DPP hana nia ya kuendelea kuwashitaki, ambao ni
Bw. Mawanda Maalo, Bw. Hawalulema Venist, Bw. Sylvester Salugo na Bw. Mohamed Simbwa Mohamed.

 

 

 

Uamuzi wa DPP wa kuwafutia washitakiwa wanne pia uliambatana na uamuzi wa kuendelea kumshitaki mshitakiwa mmoja ambaye pia ni raia wa Uganda Bw. Abdul Karim Msanje, ambaye atakabiliwa na mashitaka hayo ya mauaji.

 

 

 

Mshitakiwa huyo anatumikia kifungo cha miaka 15 jela kufuatia makosa ya kupatikana na silaha pamoja na risasi ambapo alikamatwa na bunduki mbili aina ya SMG AK 47 zenye namba 1975-230912 na 56-3903138 pamoja na risasi 87 ambazo zinadaiwa kutumika kwenye mauaji ya hao askari na mbwa.

 

 

 

Watuhumiwa hao walidaiwa kuwaua askari namba D.1672 Koplo Hassan, E.7324 D/C Ramadhani na E.7999 D/C Deogratius mnamo Mei 25, 2003 huko Kawe, Dar es Salaam.

 

 

 

Mbali na kuua maaskari hao pia walidaiwa kuua mbwa wa polisi, Rogger ambao walikuwa wanatumika katika doria ya siku hiyo.

 

 

 

Ilidaiwa kuwa, majambazi hao walianza kuwafyatulia risasi polisi wakati dereva anataka kuondoa gari hivyo kupoteza mwelekeo na kuacha barabara na kupindukia mtaroni, wakati huo huo majambazi wakiendelea kufyatua risasi.

 

 

 

Mapolisi watatu walikufa papo hapo na wengine kujeruhiwa vibaya ambapo Siku chache baadaye waliwakamatwa Waganda hao kwa tuhuma za mauaji hayo.

 

 

 

Polisi pia walimpiga risasi raia mwingine wa Uganda, Bw. Emmanuel Lugema, ambaye alikuwa akituhumiwa kuwa ni miongoni mwa wavamizi waliokuwa wakijaribu kukimbia.

 

 

 

Source: Majira

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents