Waganga wa dawa za asili waandaa katiba mpya

waganga_face

Chama cha waganga na wakunga wa tiba asili Tanzania wamefanya mkutana jijini Dar es salaam kwaajili ya kujadili Katiba mpya kuwaomba waganga kujiunga na chama hicho, ambao wanatumia dawa za miti shamba wakiwa na wamasai na watu wengine.

Mwenyekiti wa chama hicho Taifa, Seleaman Iddi Ruwa, katika mkutano  uliofanyika jijini Dar es salaam ambalo ulijadili mapendekezo ya katiba  mpya ya chama hicho.

Pia aliongeza kwa kusema  wanakaribisha waganga wote na wauza dawa , wakiwa na wamasai kujiunga na chama hicho ilikuweza kutoa huduma ya kueleweka, yenye  uaminifu na uhakika.

Waganga

Alisema kwamba wanachama wa chama hicho wote wamejiorodhesha pindi wanapotoa huduma yao, kwa wateja pia wanashahada na elimu  ya tiba za asili.

Aidha amesema wao ni  tofauti na hao waganga wa mtaani ambao wanahitaji ngozi na  viungo vya mwanaadam,  kwakuwa wao wananatambuliwa na serikali na  wapo kwenye mipango ya kusajiri katiba mpya.

Amesema miongoni mwa mambo yaliyojadiliwa hapo mwanzo na yataendelea kujadiliwa hivi sasa ni, kupokea na kuidhinisha muktasari wa nyuma, kupitisha rasimu ya Katiba mpya, kupitisha kanuni za fedha, maadili na sheria  na kupitisha ratiba ya chaguzi kuu.

waganga_3

Kunzia kushoto ni mwenyekiti wa taifa Chama cha Waganga na Wakunga wa Tiba Asili Tanzania ‘CHAWATAITA’, ni Seleman Ruwa,Yakob Ahmedi mwenyekiti wa nidhamu kutoka Kagera,Mzee Issa Maramoja , Pum Manyopa katibu mwenyezi taifa, Mzee Ibrahim Kakera mwenyekiti mkoa wa Kagera

Waganga_2

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents