Wagaruka,Nzoyimana Wasajili Azam FC

TIMU mpya katika Ligi Kuu Tanzania Bara, Azam FC imezipiga bao Simba kwa kumnasa winga machachari wa Uganda, Danny Wagaluka na kiungo hatari wa APR ya Rwanda, Haruna Niyonzima aliyekuwa anatakiwa na Yanga.

 

TIMU mpya katika Ligi Kuu Tanzania Bara, Azam FC imezipiga bao Simba kwa kumnasa winga machachari wa Uganda, Danny Wagaluka na kiungo hatari wa APR ya Rwanda, Haruna Niyonzima aliyekuwa anatakiwa na Yanga.


Azam, ambayo imemaliza mzunguko wa kwanza katika nafasi ya nane ikiwa na pointi 13, inaonekana kuupania mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Bara ambao utaanza Januari 10 mwakani.


Kikosi hicho cha Mbrazili, Neider dos Santos jana kilifanya mazoezi kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam kikiwa na Wagaluka ambaye alitua nchini juzi akitokea timu yake ya Mamlaka ya Mapato Uganda (URA).


Licha ya Wagaluka ambaye huvaa jezi namba 12 katika kikosi cha URA na timu ya taifa ya Uganda, Azam pia ilifanya mazoezi na mchezaji wa Tusker ya Kenya, Osborne Monday.


"Monday na Wagaluka wamewasili na wameanza mazoezi na timu yetu katika Uwanja wa Taifa, tunafanya nao mazoezi. Wagaluka ni uhakika kuwa anasajiliwa jioni hii (jana), lakini huyu mwingine (Monday) sijajua vizuri lakini yupo," alisema mmoja ya maofisa wa Azam.


Mtoa habari huyo wa uhakika alisema kuwa jana jioni walikuwa wanatarajia kumpokea kiungo Haruna Niyonzima wa APR ya Rwanda ili kufanya naye mazungumzo kabla ya kumsajili.


Niyonzima amekuwa akiwaniwa na Yanga mara kwa mara na kulikuwa na mpango wa kutaka kumuongeza katika usajili mdogo wa ligi, lakini Azam inaweza kuwa imetibua mipango huo.


"Tumepania sana mzunguko wa pili, hatutaki masihara tena kwani tumegundua kuwa ligi ni ngumu na tunachotakiwa ni kuhakikisha tunafanya usajili mzuri," kilisema chanzo cha habari.


Kama itawapata wachezaji hao, Azam itakuwa miongoni mwa timu tishio mzunguko wa pili kwani wachezaji wote watatu ni wazuri na wenye uzoefu wa hali ya juu.


Wagaluka amekuwa akiwaniwa na Simba kwa maneno kwa miaka mitatu, huku Haruna akiwa anawania na Yanga bila mafanikio.

 

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents