Habari

Wagombea wa Trump washinda uchaguzi Marekani

Chama cha Republican cha Rais wa Marekani, Donald Trump kimeibuka washindi wa uchaguzi wa bunge la Congress.

Uchaguzi wa jimbo la Georgia ndio umeteka vichwa vingi kutokana na kugharimu fedha nyingi katika kampeni zake ambapo Bi. Karen Handel, ambaye ni mgombea wa Republican ameshinda kwa asilimia 53 ya kurra zilizopigwa huku mgombea wa Democratic akijipati asilimia 47 ya kura hizo.

Spika wa bunge la Marekani Paul Ryan alimpongeza Bi Handel kwa ushindi huo mnono ambapo mwanzoni chama cha Democratic kilitegemea kushinda kwenye uchaguzi huo kutokana na kushuka kwa umaarufu wa Trump kwenye jimbo hilo.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotoka inadai, jumla ya dola milioni 56 zinakadiriwa kutumika katika uchaguzi huo katika jimbo la Georgia na ndio inasemekana ndio uchaguzi uliogharamikiwa katika historia ya Marekani.

Na Laila Sued

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents