Habari

Wagonjwa 4,730 wapona Corona, kasi ya maambukizi yapungua kwa kasi Hubei na Wuhan

Balozi wa Tanzania nchini China Mbelwa Kairuki -Japani ilikuwa na wanafunzi pale Wuhan na wote walikuwa wazima, lile zoezi la kuwarudisha lilivyoendeshwa baadhi yao walipata virusi vya Corona, wakaambukiza wenzao watano ambao walisafiri nao

Wagonjwa 4,730 wamepona virusi vya corona (covic-19) tangu virusi hivyo viliporipotiwa kutokea miezi mitatu iliyopita nchini China.

Taarifa ya ubalozi wa China hapa nchini ilisema kuwa hadi kufikia jana zaidi ya watu 44,653 waligundulika kuwa na virusi hivyo na 4,740 kati yao walitibiwa na kuruhusiwa kurudi nyumbani.

Taarifa hiyo ilisema kuwa virusi hivyo vimesababisha vifo vya watu 1,113 na 38,800 wakiendelea kupatiwa matibabu katika maeneo mbalimbali ya ndani na nje ya nchi hiyo.

“Watu wengine 16,067 wanahofiwa kuambukizwa virusi hivyo ambako sasa wameweka katika maeneo maalum kwa ajili ya uchunguzi.

“Habari njema ni kwamba idadi ya visa vipya sasa imepungua kwa kiasi kikubwa katika eneo la Hubei, Wuhan ambako ndiyo chimbuko la ugonjwa huo,” ilisema taarifa hiyo.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, ugonjwa huo umesambaa katika nchi 27 duniani zikiwamo Uingereza, Marekani, Japani na Korea Kaskazini.

Hata hivyo, taarifa hiyo ilisema Watanzania waliopo nchini humo wako salama.

“Tuna shirikiana vizuri na balozi wa Tanzania nchini China, Mbelwa Kairuki kuhakiksiha wanafunzi wote wa Kitanzania wanaoishi katika mji wa Wuhan wanapatiwa msaada wa hali na mali.”

Taarifa hiyo ilisema kwa sasa ni vyema wanafunzi hao wakabakia nchini China kama ilivyo shauriwa na Shirika la Afya Dunia (WHO), ili kuepusha kuendelea kueneza ugonjwa huo katika mataifa mengine.

Katika hatua nyingine, WHO imetangaza jina rasmi la ugonjwa huo unaosababishwa na maambukizi ya virusi vya corona kuwa ni Covid-19.

Akitoa taarifa kwa waandishi wa habari mjini Geneva, Uswizi Mkurugenzi Mkuu wa WHO, Dk Tedros Ghebreyesus alisema wamepata jina rasmi la ugonjwa huo baada ya wataalam wa afya kufanya uchunguzi.

“Sasa ugonjwa huo utafahamika kwa jina la covid-19,” alisema mkurugenzi huyo. Tedros alisema co inawakilisha corona, vi ikiwa na maana ya virusi, d ikisimama badala ya ugonjwa huku namba 19 ikiwakilisha muda ambao ugonjwa huo ulilipuka mwaka 2019.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents