Jiunge ufaidi miezi 2 bure!

WaGoSi na nyie kwa kupakaza!!

Kundi la Wagosi wa Kaya ambalo mara zote limekuwa likiheshimika na jamii kwa nyimbo zao ambazo kwa namna moja au nyingine zimekua zikiilenga jamii na mafundisho ya kutosha…wamerudi tenaa safari hii na songi liitwalo (TAARIFA YA HABARI).

Mkoloni

Wakiwa tayari wameshatamba sanaaaa na vibao kama ‘Tanga kunani’, ‘Wauguzi’, ‘Trafiki’, ‘FAT na vinginevyo..wasanii hawa wanasema songi hili linakuja mahususi kwa ajili ya kuja kuipasha jamii juu ya matumizi mabaya ya nyumba za kulala wageni yaani GUEST HOUSE.

Akizungumza mwishoni mwa wiki iliyopita, mmoja wa wasanii wanaounda kundi hilo anayekwenda kwa jina la Mkoloni,alisema songi hilo linazungumzia ongezeko la nyumba za kulala wageni ambazo ni maarufu kama ‘gesti bubu’ ambazo haziko maalum kwa ajili ya kulaza wageni kama ilivyotarajiwa, na badala yake hutumika kufanyia ngono tena zingine zisizo salama kitu ambacho ni hatari kwa jamii haswahaswa kipindi hichi ambacho kuna janga kubwa la UKIMWI.

  • SOURCE: Darhotwire

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW