Habari

Wahalifu waendelee kuwa na hofu – Kamanda wa polisi Kinondoni

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Jumanne Muliro amesema kuwa hali ya ulinzi na usalama katika uchaguzi unaoendelea Kinondoni uko imara.

Akizungumza muda huu Kamanda Muliro amesema kuwa wale wote wenye haki ya kupiga kura wanafurahia hali ya usalama huku akieleza kuwa hakuna anae watisha bali ni haki yao Kikatiba.

Hata hivyo Kamanda wa Polisi alipoulizwa wingi wa askari katika vituo hauwezi kuwa letea wananchi nchi hofu? Kamanda Muliro amesema kuwa watu wanaotishika ni watu ambao sio wema huku akieleza kuwa watu walio wema wanatamani askari waongezeke zaidi ya hapo.

Aliongeza kuwa wahalifu waendelee kuwa na hofu huku akiwataka watu wema kuendelea kufuahia ulinzi na usalama.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents