Habari

Wahamiaji haramu 36 raia wa Ethiopia na Somalia wakamatwa Dar, RC Kunenge atoa onyo kali (Picha)

Vyombo vya ulinzi na usalama Mkoa wa Dar es salaam vimefanikiwa kuwatia mbaroni Wahamiaji haramu 36 raia wa Ethiopia na Somalia walioingia nchini kinyume na taratibu ambapo Mkuu wa Mkoa huo Mhe. Aboubakar Kunenge ametoa onyo Kali kwa Raia wa Tanzania wanaoshiriki kuwafadhili na kuwasafirisha kwa ili wapate fedha.

RC Kunenge amesema Wahamiaji hao walikamatwa usiku wa kuamkia November 15 kwenye fukwe za Mbweni ambapo kati yao 30 wanatoka nchini Ethiopia na Sita wanatokea nchini Somalia.

Aidha RC Kunenge amesema hata utaratibu unaotumika kusafirisha watu hao unakiuka Sheria, haki na utu wa binadamu sababu wengi wao wanafungiwa kwenye kontena zisizokuwa na hewa na pindi wanapobainika kufariki Dunia maiti zao hutupwa kwenye vichaka.

Pamoja na hayo RC Kunenge amevipongeza vyombo vya ulinzi na usalama kwa kazi kubwa na nzuri wanayoifanya.

Kwa upande wake Afisa uhamiaji Mkoa wa Dar Es Salaam Kamishina Msaidizi Edmund Mrosso amesema kinachofuata baada ya wahamiaji hao kukamatwa watafikishwa Mahakamani kwa kosa la Kuingia nchini kinyume na taratibu.

Aidha Kamishina Mroso amesema kwa wale wanaowasafirisha au kuwahifadhi wahamihaji hao adhabu inaelekeza kifungo Cha miaka 20, faini ya shilingi milioni 20 au vyote kwa pamoja ikiwa ni pamoja na kutaifisha mali zilizotumika.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents