Wahandisi wa maji wanyooke na asiyekubali kunyooka tutamnyoosha – Mh. Aweso (+video)

Serikali imewaagiza wahandisi wote wa Wizara ya Maji ambao wamehamia katika wizara hiyo kwamba wanatakiwa kunyooka na asiyekubali kunyooshwa atanyooshwa.

Kauli hiyo imetolewa na Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Jumaa Aweso wakati akijibu swali la Mbunge Lucy Simon Mbunge wa Viti Maalum,

Je, Serikali imeshawajibisha kampuni ya serengeti inayojenga mradi wa Maji wa Mpera na Kimbiji? Na Je, ni lini mradi utakamilika ilikuondoa adha kwa wananchi wa Kigamboni ambao wengi wao wanatumia maji ya visima vifupi na yasio salama?

“Naomba nitoe shukrani zangu za dhati kwa Mh. Rais, Dkt. John Pombe Magufuli kwa kusikia kilo cha waheshimiwa Wabunge kuhusu suala zima la utekelezaji wa miradi vijijini na ameagiza Wahandisi wote wote waje katika wizara ya Maji, nataka niwaambie waandishi wa maji wanyooke na asiyekubali kunyooka tuko tayari kumyoosha,” amesema Aweso.

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW