Burudani

Wahu akanusha kumsaliti Nameless, asema ni baba mzazi wa mtoto wake wa pili

Muimbaji wa Kenya, Wahu amelazimika kukanusha tetesi za kuwa Nameless si baba mzazi wa mtoto wao wa pili, Nyakio, aliyezaliwa mwaka jana.

1921947_10152264642969228_1783972085_n

Katika mahojiano aliyofanya hivi karibuni, Wahu alisema Nameless ni baba wa watoto wake wote wawili na kwamba ataendelea kuwa baba yao.

“Ndio, kuna muda ndoa yangu ilikuwa matatani. Sisi ni wapenzi wa kawaida na hukabiliana na masuala kama wapenzi wengine, lakini nielewe, huko kulikuwa kutokuelewana tu na hakuna kitu kama talaka kilikuwa kitolewe,” alisema. “Tulitofautiana kwenye masuala kadhaa lakini tuliyamaliza. Ingawa tulikuwa tumekasirikiana kipindi hicho, bado tuliendelea kuongea tofauti na wapenzi wengine ambao hushindwa kuongea kwa wiki ama miezi licha ya kuishi pamoja. Tunamshukuru Mungu kuwa yote yapo nyuma yetu sasa. Tuko imara kuliko zamani na tafadhari, baba wa watoto wangu siku zote ataendelea Nameless.”

Chanzo: Ghetto Radio na Vibeweekly

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents