Picha

Waingereza wajipanga kusherehekea birthday ya miaka 90 ya Malkia Elizabeth

Sherehe kubwa ya siku tatu mfululizo ya birthday ya Malkia Elizabeth II itaanza Jumamosi hii nchini Uingereza.

stream_img (1)

Tarehe rasmi ya kuzaliwa kwa malkia huyo ni 21 April, 1926, ambapo alifikisha miaka 90.

Lakini huwa na tarehe tofauti ya kusherehekea siku yake hiyo ambayo mwaka huu itakuwa ni June 11. Ni kwasababu June ni mwezi ambao hali ya hewa ya Uingereza huwa nzuri zaidi.

Elizabeth na mume wake Prince Philip watahudhuria misa ya shukrani kwenye kanisa la St. Paul ijumaa hii ambapo Philip anasherehekea miaka 95 ya kulizaliwa. Kesho kutachangamka zaidi kwa parade maalum kwenye ikulu ya Buckingham.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents