Habari

Waislamu kote duniani washerehekea sikukuu ya Eid

Waislamu kote duniani leo wanasherehekea sikukuu ya Eid ul-Fitr huku wengi wakiwa chini ya vizuizu vilivyowekwa na mataifa kukabiliana na kuenea kwa virusi vya corona.

Sikukuu ya Eid moja ya sherehe muhimu kwenye kalenda ya uislamu huashiria kumalizika kwa mwezi mtukufu wa Ramdhan na huadhimishwa kwa ibada ya swala, dhifa za chakula na manunuzi ya zawadi pamoja na mavazi.

Hata hivyo mwaka huu sherehe za Eid zinaandamwa na kiwingu cha janga la corona huku nchi nyingi duniani zimetangaza kurejesha vizuizi ambavyo kwa sehemu vililegezwa wakati wa mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhan.

Katika hali ya kupunguza msisimko wa sherehe hizo mataifa kadhaa ikiwemo Saudi Arabia, Uturuki, Misri na Syria yamepiga marufuku ibada za umati, moja ya tukio muhimu katika sikukuu ya Eid, kwa lengo la kuzuia kusambaa virusi vya corona

Nchini Saudi Arabia, yaliko maeneo mawili tukufu kwa dini ya Uislamu, serikali imetangaza kuwa swala ya Eid itafanyika kwenye misikiti mikuu ya Makka na Madina bila kuhudhuriwa na waumini.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents