Burudani

Wajanja wajaribu kumtapeli Bob Junior

Imebainika kuwa kuna mtu aliyetengeneza line mpya kwa kutumia namba ya Bob Junior aliye barani Ulaya kwa sasa na kutaka kuwatapeli watu wake wa karibu kuwa hitmaker huyo wa Nichum yupo hoi na anahitaji msaada haraka.

72910_10151418615904962_719201817_n

Taarifa hiyo imetolewa na baba yake mdogo, Guru Ramadhan ambaye ni mmiliki wa G Records. Kupitia Facebook, Guru aka G Lover ameandika:

“Hii sijaipenda kabisa ni too much sasa..eti mtu yupo Europe na simu yake inaita bongo ukipiga duh kumbe mtu katengeneza line mpya na kutumia namba ya Bob Junior na pia jamaa anayetumia hiyo line ya simu eti anaomba msaada kwa watu kuwa Bob Junior anaumwa sana Ulaya anahitaji msaada wako ili arudi Bongo.

Hivi nini maana ya kusajili namba?…makampuni ya simu ya Bongo mjipange sanaaa…hili limemkuta msanii Bob Junior siku chache hizi, mpaka imeripotiwa polisi eti ndio wamejidai kui block number…t.g. mmeniboaje?..so guyz mnaosafiri muwe makini sana mkisafiri maana mnaweza kukuta madeni kibao mkafa na presha bure…wizi mtupu…I hate dat.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents