Burudani

Wajua kuwa Ditto na Amini wana kampuni ya uandishi wa nyimbo, matangazo na vitu vingine? Inaitwa Green Light Music and Company

Kadri miaka inavyoenda, ndivyo wasanii wa Tanzania wanaendelea kufikiria nje ya box na kuacha kutegemea tu shows ama malipo mengine kutokana na muziki wao ili waendeshe maisha yao.

1004861_10201355844371300_125219477_n

Unaweza ukawa huwasikii wakitoa nyimbo mara kwa mara, ama huwasikii wakitajwa kutumbuiza kwenye show mbalimbali lakini ukikutana, utagundua kuwa maisha yao ni mazuri na hawalalamiki.

Ndivyo ilivyo kwa Ditto. Yeye pamoja na Amini wana kampuni yao iitwayo ‘Green Right Music and Company’, ambayo kutokana na majukumu yake, imemfanya Ditto asiachie nyimbo mara kwa mara.

“Ukimya huu mambo yanaenda ipo kampuni inaitwa GREEN LIGHT MUSIC AND COMPANY mimi ndio ambaye naiendesha lakini Share holder ni Amini,”Ditto aliiambia ‘Chumba Cha Sindano’ upitia kipindi cha Kali za Bomba cha kituo cha redio, Bomba FM Mbeya.

“Tumekuwa tunajishughulisha na masuala mengi ya uandishi wa nyimbo, ku-create kampeni tofauti za makampuni mengine mengine, ringtones, vipindi vya TV na yaani mambo mengi ambayo tumekuwa tunayafanya lakini asilimia nyingi pia matangazo kwa sababu napiga katika redio ujue sisi ndio tunayafanya. Kwa hiyo watu wasione ukimya kuna shughuli nyingine naendelea nazo huku chini naifanya nyingi tu bado naendelea kuzitumia variety za muziki katika kufanya shughuli nyingine.”

Katika hatua nyingine, Ditto alisema sababu zinazomfanya azirudie kuziimba za nyimbo za zamani maarufu kama Zilipendwa, ni kuwafanya wadau wa muziki kuzikumbuka na kuzisikiliza kutokana na kuwa na ujumbe wenye mafunzo ya kimaadili ndani ya jamii.

By Greyson Chris Bee (Bomba FM)

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents