Burudani

Wakali wa Oga Police na Loke ‘Shiikane’ kutua Tanzania

Kundi la Muziki la Shiikane linaloundwa na wasanii watatu kutoka Nigeria,  HrH Shay, Princess Annamay na Baby-K, linatarajia kutua nchini Tanzania mwaka huu kwaajili ya kufanya media tour pamoja na kufanya promotion ya wimbo wao mpya ‘Oga Police’.

Wasanii wa Kundi la Shiikani

Mrembo hao ambao makazi yao ni Uingereza na Nigeria wanafanya kazi chini ya label M.A Records na wameandaa kampeni yao  ya #ogapolice#tanzaniatour kwaajili ya kutoa zawadi mbalimbali za hela kwa washindi nchini Tanzania.

Shiikane ambao ni washindi wa tuzo ya BEFFTA Awards 2015 – Best Music Video kupitia video yao ya wimbo ‘Tuele’ wanaonekana kuwa ni kundi la wasanii wa kike ambalo linakuja kwa kasi zaidi barani Afrika.

Wakali hao wa kuimba ambao kwa sasa wanafanya vizuri na video ya wimbo ‘Oga Police’ wanakuja Tanzania baada ya kuona kuna mashabiki wengi wanaoufuatilia muziki wao kwa ukaribu zaidi.

Wasanii hao wamewataka mashabiki wa muziki nchini Tanzania kujirekodi clips za video wakicheza wimbo ‘Oga Police’ na then kuzituma whatsapp kwa mamba 0785272727 ili kujishindia zawadi mbalimbali.

Mshindi wa kwanza kupitia shindano hilo atajinyakulia kitita cha tsh milioni moja, wa pili atajinyakulia tsh laki tano na mshindi wa tatu anajinyakulia kitita cha tsh laki tatu taslimu.

Pia warembo hao wakija Tanzania watafanya jitihada za kufanya kolabo na wasanii wa ndani ili kupata ladha tofauti katika muziki wao.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents