Habari

Wakamatwa na fedha bandia dola Mil. 10, walaghai watu kwa kudai wakiwaombea pesa zao zinakuwa mara mbili ya zile

Raia wawili wa Chad na mmoja wa Kenya wamekamatwa na Jeshi la Polisi nchini Kenya wakiwa na zaidi ya dola milioni 10 ambazo ni fedha bandia.

Akidhibitisha tukio hilo Mkuu wa kitengo cha flying squad, Musa Yego amsema Abdoulaye Tamba na AbdallaTamba kutoka Chad wamekuwa wakiwaambia wateja wao kuwa wanaweza kuwaombea wapate utajiri.

“Tumewakamata vijana watatu wa kiume wanaojulikana kwa majina, Abdoulaye Tamba, Abdalla Tamba wote raia wa Chad na Anthony Mwangangi wa Kenya ambaye yeye ni dereva wao,” amesema Mkuu huyo Musa Yego .

Vijana hao wawili raia wa Chad wamekuwa wakiwaambia watu kuwa wanauwezo wa kuwaombea watu na fedha zao zikawa mara mbili ya walizonazo kupitia ushirikina.

Yego ameongeza kuwa Wachad hao wamekuwa nchini Kenya kwa zaidi ya miaka 10 na wanamtafuta mmiliki wa nyumba waliyokuwa naishi vijana hao kwa mahojiano zaidi ili kujua kama anafahamu nini juu ya raia hao wa kigeni.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents