Habari

Wakati unatafuta furaha: Upende kitu unachofanya

Je ni kitu gani ambacho kinaweza kutusaidia kwenda hatua nyingine katika maisha ya kila siku na kitaaluma? Kwa uelewa wangu binafsi, ni kupenda unachokifanya. Wakati natafuta furaha, haya ni baadhi ya mambo ambayo ninayaangalia.

Kutengeneza mpangilio katika taaluma yangu.

Kama ninapenda ninachofanya, ninarahisisha mambo mengi, nitabadilisha namna ninavyofanya kazi na kutafuta watu sahihi ili niweze kufanya kazi ambayo mimi peke yangu siwezi. Hili jambo linawezekana kama unapenda unachofanya.

Katika Ufanisi  na Utendaji.

Kwasababu unapenda unachofanya hata ufanisi unaongezeka. Wakati wote unatafuta namna ya kuboresha unachokifanya, kwasababu hufanyi kwa ajili ya watu wengine bali kwaajili  yako mwenyewe, na hilo huleta matokeo tofauti na bora zaidi.

Mahusiano yako na watu yanakuwa bora zaidi

Tunasikia kuhusu siasa, kazi zinapokuwa nyingi ofisini, mabosi kunyanyasa wafanyakazi wao n.k. Mambo hayo huwa mara nyingi yanakuwa rahisi kwa mtu anayependa anachokifanya, vitu vingi unakuwa unafanya bila kusukumwa na mtu. Inamaanisha unakuwa na uhusiano wako mzuri na bosi wako kwani kazi yako inafanyika kwa wakati na ubora sahihi kwa sababu unapend na kile unachokifanya.

Kwa kawaida ninamaanisha kutoacha nafasi ya kile tunachokipenda na kupenda kile tunachokifanya.Kama tunataka kuwa na furaha na kufurahia kile tunachokifanya itatufanya kuwa watu bora zaidi kwenye maisha binafsi na hata maisha ya kitaaluma.

Inaonekana kana kwamba haiwezekani, lakini inawezekana. Uwezo wako wa kupenda kufanya kitu unatakiwa uwe zaidi ya vikwazo unavyokutana navyo ofisini au kwenye biashara. Hivyo chagua kazi unayoipenda na hautakuja kufanya kazi tena maishani mwako, kwani kazi yako itakuwa ni maisha yako na si kazi kama kazi.

Awali Mwaisanila

A Personal Career Development specialist, passionate about empowering emerging generations of student, graduates and working class.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents