Burudani

Wakazi amkingia kifua Chid Benz, ‘ishu ya unga inatoka wapi?’

Msanii wa hip hop Bongo, Wakazi ameonyesha kutopendezwa na wale wanaomsema vibaya rapper Chid Benz kutokana na clip ya video inayosambaa mtandaoni.

Clip hii ya video ambayo ni mahojiano aliyofanya Chid Benz na E-Newz ya EATV alisema amezungumza na Tupac na wamepanga kufanya ngoma wakati msanii alishafariki kitu ambacho kimeibua mshangao mkubwa. Kupitia Instagram Wakazi ameandika;

Hiyo clip ya Chidi Beenz mbona wengine moja kwa moja mmeanza kumjaji ?! Issue ya Unga inatoka wapi?! Kama alichoongea mnahisi ni that disturbing basi mtafutieni msaada kwanza kabla ya kumhukumu. Lazima tuweke mezani all possible options kabla ya kupitisha moja kwa moja judgement, tena ambayo our course of actions after it ni kutikisha kichwa na kusema “Dah” au “Maskini Chidi” badala ya kumkwapua from that condition.

Yes inawezekana alichoongea ni ishara ya mental instability, ila hakina tofauti na Dayna Nyange kusema “Drake ni shemeji yake”, au Young Dee kusema “Atachukua RB kwa mtu aliyevujisha Picha zake za Uchi alizopiga mwenyewe kwa hiari”. Je kama Chidi ameamua kutafuta Kiki kwa kufanya kitu outrageous and divert the attention from SeduceMe/Zilipendwa By Ali Kiba & Diamond ?!

That’s the name of the Game right?! Kiki alafu unafata muziki au sio?! And by the way, hip hop community ya marekani huwa yote inasemaga “Tupac is in Cuba” sio Eminem sio Kendrick Lamar!! A drug addict is a patient, so is a Mentally unstable person. The former can birth the latter. Chidi zima Kiki Washa muziki, maana muziki unauweza haswa!! Ila kama hii ni an indirect cry for help, I’m urging everyone to do just that. © BEBERU

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents